Katika hali isiyo ya kawaida kutokea kwenye mikutano ya injili,watumishi wa
muhubiri mwenye jina kubwa nchini Josephat Gwajima wamemshambulia kwa kipigo
kikali kijana mmoja Elias Mokiwa mshirika wa kanisa la Assembles of God (TAG)
Elias Mokiwa kwa kudaiwa kutenda kosa ya kuipiga picha misukule inayodaiwa
kurudishwa kupitia huduma hiyo.
Tukio hilo lililowashangaza watu wengi hata wale wasio wakristo lilitokea jumapilki ya tarehe 1 mwezi Novemba kwqenye viwanja vya Tangamano wakati muhubiri Gwajima akiwa anaendelea na mahubiri yake ya kuwaita misukule "njoooooo" na kuwasadikisha watu kuwa kw akuita huko misukule popote ilipo inakuja yenyewe hadi uwanjani hapo.
Mahubiri hayo kwa kiasi kikubwa yakivuta idadi kubwa ya watu kwenye viwanja hivyo wengi wao wakija sio kwa sababu ya kusikia injili iokoayo wala hakukuwa na nafasi ya watu kutubu dhambi kama Bwana Yesu alivyosema alivyoanza huduma yake 'tubuni na kuiamini injili kwakuwa ufalme wa Mungu umewajilieni'bali watu hao walifika kwa kutaka kuona misukule hiyo.
Katika mvuto huohuo wa misukule alipoanguka mama mmoja aliyedaiwa kuwa ni msukule kijan a Elias ambaye anasomea chuo cha uandishi wa habari cha Royal jijini Tanga,alishawishika kupiga picha ndipo alipogundulika na wahudumu wa Gwajima na kupokea kibano hicho kutoka kwa watu walioonekana hawana hata huruma ya kimungu ndani yao.
Elias mwenyewe akizungumzia tukio hilo kwa wandishi wa habari alisema kuwa baada ya kukamatwa akipiga picha, alichukuliwa na kupelekwa nyuma ya jukwaa wakamvua mkanda ambao ulitumika kumfunga mikono yake yote miwili kwa nyuma na kisha kumpa kipigo kama mwizi.
"Nilishambuliwa kwa mateke ngumi na magongo..kwakweli najiskia maumuvu sana tangu saa 12 waliponikamata waliniachia saa mbli usiku nikiwa nyuma ya juukwaa mahali ambapo watu wengi walikuiwa hawaoni tukio hilo isipookuwa mwanachuo mwenzangu mmoja anayeitwa Veronica Mboto ndiye aliyeshuhudia na kutoa taarifa iluyopekea baadae kuokolea kutoka eneo hilo nililoliona kama kuzimu."alisema.
Kamanda wa polisi mka wa Tanga Constatine Massawe alipopewa taarifa hiyo alijibu kwa njia ya simu kuwa yuko safarini, lakini alisema kuwa kama kweli itathibitika watuhumiwa watachukuliwa hatua kama wahalifu wengine. na akaagiza suala hilo lipelekwe kwa Mkuu wa kitengo cha upelelezi wa makosa ya jinai mkoa (RCO).
Tayari sakati hilo liko mikononi mwa polisi mkoa wa Tanga na limefunguliwea jarada la upelezi (file) PE 71 2013,
ambapo bado upelelezi wake unaendelea.
Mkuu wa kitengo cha upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Tanga (RCO) Azizi Kimata alisema kuwa watachukua hatua baada ya upelelezi wa awali kukamilika.
Baadhi ya wakristo waliohojiwa na gazeti hili walionekana kushangazwa na tukio hilo kwani haijawahi kutokea kwa wahudumu wa mkutano wa injili kupiga watu kama ilivyotokea wakati huu.
"Sisi wakristo ikitokea miujiza kwenye mkutano wa injili tunawaita waandishi wa habari waje watangaze kwani huo ni ushuhuda KWA watu wengine wajue kuwa Mungu wetu anaweza. ..sasa hawa wenzetu wanadai kufufua misukule ambao ni muujiza mkubwa halafu hawataki waandishi kuwapiga picha na kuwatangaza, tuna wasiwasi na miujiza hiyo kama ni misukule ya kweli au feki' alisema mtumishi mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment