Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema kuwa Hayati Nelson Mandela
atazikwa tarehe kumi na tano Jumapili mwezi Disemba katika eneo la Qunu
mkoa wa Estern Cape.
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete,
ametangaza siku tatu za maombolezi, kufuatia kifo cha mzee Nelsomn
Mandela, akisema kua Afrika na dunia nzima kwa ujumla imempoteza shujaa
mkubwa sana katika karne ya 20 na 21.
Kikwete alisema kupitia taarifa kwa vyombo vya
habari kua Mandela ni kiongozi wa kipekee na mtu aliyeenziwa sana na
dunia nzima pamoja na watu wa Afrika Kusini baada ya kupigania sana
demokrasia nchini Afrika Kusini.Kwa upande wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, amesema kuwa Mandela alikuwa mfano mzuri wa umuhimu wa kuwa na matumaini na kuwataka watu kuwa na uelewa wa kuwasamehe bila masharti wale wote wanaotukuosea.
Naye Rais wa Rwanda Paul Kagame,amesema kua Mandela ataendelea kuishi kwenye mioyo ya wengi wetu.
Naye Rais mstaafu Daniel Moi ambaye alikuwa madarakani wakati Mandela alichaguliwa kuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, amempongeza Mandela kwa kuhakikisha utulivu wa kisiasa barani Afrika na kuwa mfano bora kwa viongozi wengine.
No comments:
Post a Comment