..

..
.

Friday, December 6, 2013

COSTAL UNION KUANZA MAZOEZI RASMI DESEMBA 9

Jana nilizungumza na mwalimu wa Coastal Union, Yusuf Chippo ameniambia mazoezi yataanza rasmi siku ya Jumatatu Desemba 9 (siku ya uhuru). Tayari wachezaji wameshaanza kuripoti na ambao hawajaripoti wawasiliane na Meneja Akida Machai ama Katibu Kassim Siagi, wapewe maelekezo.

Vilevile Taarifa kuhusu usajili wa dirisha dogo, kazi hiyo tumemuachia Mwalimu, yeye ndiye atajua wapi pamelegalega aongeze nguvu. Tunajua dirisha dogo linafungwa Desemba 15, hii wiki moja inatosha kwa mwalimu kukijua kikosi chake.

Aidha kuhusu safari ya nje ya nchi, kwa mujibu wa Katibu safari ya Oman imeshaiva, wenyeji wetu Fanja FC wamekubali kutupokea, sasa kinachofuata ni utaratibu wa kupata Visa (Viza).

Siku na tarehe ya kuondoka tutawajulisha baada ya utaratibu wa visa kukamilika. Ila tunajua ligi inaanza Januari 25 katika uwanja wa Mkwakwani tutacheza na JKT Oljoro, kwahiyo tutakwenda Oman mapema ili tuwahi mechi.


No comments:

Post a Comment

KARIBU