..

..
.

Friday 6 July 2012

MTANZANIA AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA, HOUSTON, TEXAS




Vipipi vya madawa ya kulevya  vyenye uzito wa karibu pound 5, vilivyokamatwa mwezi March, Dulles International Airport Viginia kutoka kwa mwanamke Mnigeria.

Bryan Mukama Hans, 30, Mtanzania aliyekua amekuja Marekani na VISA ya kutembea kwenye Family Re-Union alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kushikiliwa na Polisi wa Uwanja wandege wa kimataifa wa George Bush, Houston, Texas baada ya kupatikana amemeza vipipi vya madaya ya kulevya vifikavyo 100 vyenye uzito karibia pound 3.

Bryan Mukama Hans alikamatwa Mwezi uliopita baada ya kushukiwa alipokua na wasiwasi mwingi, midomo mikavu na alipokua akiulizwa maswali na uhamiaji alijibu huku akikwepesha macho na kudai alikua yupo njiani kuelekea Utah kuungana na familia yake kwenye Family Re-Union na mmoja ya wanafamilia alithibitisha kuwepo wa family Re-Unioni hiyo iliyokua ifanyike July 4, siku ya Uhuru wa Marekani na sio June kama alivyokua akidai Hans.

Baada ya kufanyiwa X-ray ya tumbo, Hans aliomba kutumia choo na kutoa vipipi 22 vilivyopimwa na kuthibitika kwamba ni Heroin na baadae alipelekwa Hoston Northwest Medical Center na kutoa vipipi vingine 78


Hii ndio Houston Northwest Medical Center alipoletwa Bryan Mukama Hans kumalizia kutoa vipipi 78 vingine vilivyokua vimebaki tumboni.

Bryan Mukama Hans alisema anafanyakazi ya kuuza magari Tanzania lakini mmoja ya mwanafamilia aishie Utah alisema ni mfanyabiashara anaemiliki Duka pia Hans tiketi yake ilionyesha kuishia Houston na sio Utah pia tiketi ilionyesha alitakiwa kurudi Tanzania June 18, siku 16 kabla ya family Re-Union.

No comments:

Post a Comment

KARIBU