Sekeseke la usajili limeendelea kupamba moto.
Katika kuhakikisha wanaibomoa kabisa
safu ya ushambuliaji wa watani wao iliyowafunga kipigo cha aibu cha
mabao 5-0 katika mechi ya kufunga msimu uliopita. Klabu ya bingwa ya
afrika mashariki na kati, Dar Young Africans inakaribia kumnasa
mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda na tegemeo la klabu ya Simba,
Emmanuel Okwi.
Taarifa za udaku nilizozipata kutoka
ndani ya Yanga ni kwamba timu yao ipo tayari kulipa fedha wanazozitaka
Simba ili kuweza kupata huduma za Okwi msimu ujao. Taarifa zinasema
kwamba Okwi ambaye kwa sasa yupo nchini Uganda anatarajiwa kutua
Tanzania ndani ya kipindi cha masaa 72 kuja kumaliza suala la usajili
wake kwenda Yanga ambao inasemekana wamemuhaidi fedha nyngi sana.
________________________________________________________________________
No comments:
Post a Comment