..

..
.

Thursday 7 June 2012

EURO 2012: ITALIA NA SAFU YA USHAMBULIAJI YA WENDAWAZIMU CASSANO NA BALOTELLI

Maneno ya Cesare Prandelli alipomrithi Marcello Lippi kama kocha wa timu ya taifa baada ya kombe la dunia mwaka 2010 ni kwamba ataifanya Azzuri ivutiwa kwa kucheza soka zuri la kushambulia. Kwa hakika amejitahidi sana huku akitambulisha utaratibu wa 'ethical code' (wachezaji wanaokuwa wamesimamishwa kwa makosa ya kinidhamu hawatoitwa timu ya taifa) na kusisitiza katika kuwapa nafasi zaidi viungo wenye ufundi zaidi katika timu yake. Wazo ni kuifanya Italia kucheza kwa staili yake ya mfumo wa tiki-taka, staili inayopendelewa zaidi na Wahispania.
Akiuacha mfumo wa siku nyingi wa kujenga ukuta wa chuma na kucheza kwa mashambulizi ya kushtukiza kwa ajili ya mfumo ambao unatumia na Spain, ambao mpaka sasa umeleta matokeo ya mchanganyiko. italy haikufungwa hata mechi moja kwenye hatua ya kufuzu, lakini wamekuwa wakifungwa kwenye mechi za kirafiki. Skendo ya upangaji wa matokeo ambayo inaliandama soka la nchi hiyo kwa miaka mingi sasa, haitegemewi kuwa na madhara makubwa sasa hivi kuliko ilivyokuwa katika miaka 1982 na 2006, sababu kubwa ni kwa kuwa ni wachezaji wachache wa kikosi cha sasa wameguswa na kashfa hiyo, lakini suala hilo bado linabakia kuwa sio zuri kwa wachezaji.
Droo ya group C haikuwa nzuri kwa Italy, lakini atleast mechi yao dhidi ya Spain itakuwa ya kwanza. Na kupata pointi kutoka kwenye mechi hiyo ni jambo ambalo linawezekana, kwa kuangalia Spain huwa na kawaida ya kuanza vibaya michuano mikubwa, ukiangalia kombe la dunia lilopita walipofungwa na Uswis katika mechi ya kwanza makundi. Baada ya mechi hiyo atleast kidogo mambo yanaweza kuwa mazuri dhidi ya Croatia na Ireland.

No comments:

Post a Comment

KARIBU