GAMBIA KUWASILI LEO USIKU
Timu
ya Taifa ya Gambia (The Scorpions) ambayo awali ilikuwa iwasili nchini leo
(Juni 7 mwaka huu) saa 1.40 asubuhi sasa itawasili leo saa 9.20 usiku kwa ndege
ya Kenya Airways tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars.
The
Scorpions ilipaswa kubadili ndege Dakar, Senegal jana usiku lakini kukawa na
ucheleweshaji (delay), hivyo ikashindwa kuwahi Nairobi, Kenya ambapo
ingeunganisha kwa ndege ya alfajiri kuja Dar es Salaam.
Kikosi
cha timu hiyo chenye wachezaji 22 wakiwemo tisa wanaocheza mpira wa kulipwa nje
ya nchi hiyo kitafikia kwenye hoteli Sapphire iliyopo Mtaa wa Lindi na Sikukuu
eneo la Kariakoo.
Wachezaji
walioko katika msafara huo ni Musa Camara, Abdou Jammeh, Momodou Futty Danso, Lamin
Basmen Samateh, Ousman Koli, Pa Saikou Kujabi, Mustapha Kebba Jarju, Yankuba
Mal Ceesay na Demba Savage.
Wengine ni Saihou Gassama, Alieu Darboe, Momodou
Ceesay, Pa Modou Jagne, Tijan Jaiteh, Bubacarr Sanyang, Christopher Allen, Musa
Yaffa, Sulayman Marr, Mamut Saine, Hamsa Barry, Ali Sowe, Omar Colley na Saloum
Faal.
PROGRAMU YA MAZOEZI YA GAMBIA
IJUMAA JUNI 8
01.00
asubuhi Mazoezi- Uwanja wa Karume
10.00
jioni Mazoezi- Uwanja wa Taifa
JUMAMOSI JUNI 9
04.00
asubuhi Mkutano na Waandishi wa Habari-
Ukumbi wa TFF
No comments:
Post a Comment