..

..
.

Thursday, December 5, 2013

Wezi wamkosesha raha Izzo Bizness baada ya kumuibia vifaa vya Internet Cafe yake iliyopo Mkoani Mbeya

 Rapper na Mjasiriamali Emannuel Simwinga aka Izzo Bizness hivi karibu alipata hasara kubwa kwenye Internet Cafe iliyopo Mkoani Mbeya,baada ya wezi kuvunja na kuiba vifaa vya internet Cafe vikiwemo Computer sita zinazogharimu jumla ya shillingi za Tanzania 2,700,000.
Kupitia kwenye instagram amepost picha ya Internet Cafe na kuandika jinsi alivyopokea taarifa za kuibiwa vifaa vyake na kuwataka wananchi wamsaidie.
  ' Leo ni siku mbaya sana kwangu na familia yangu pia nimepata taarifa za kuvunjiwa na kuibiwa computer sita katika ofisi yangu iliyopo mbeya maeneo ya chuo cha (TEKU) naomba mungu unitie nguvu kama upo mbeya na ukasikia watu wanauza computer pasipo njia halali tafadhali naomba utoe taarifa kwa kunijuza. Mungu abariki siku yako.

No comments:

Post a Comment

KARIBU