..

..
.

Saturday, 20 July 2013

Mahakama Kuu Mpya huko Garissa yaboresha raia kupata haki

Toka Mahakama Kuu katika jimbo la Kaskazini Mashariki la Kenya kufungua milango yake kwa wananchi mwezi Februari, serikali imeendeleza uwajibikaji wake katika kugatua huduma na kuleta haki kwa Wakenya wote.
Jaji Stella Mutuku, ambaye aliteuliwa kwenda Mahakama kuu ya Garissa, alisema Mahakama hiyo ilianzishwa kama sehjemu ya jitihada za serikali kuleta utawala wa haki karibu na watu kwani jimbo la Kazkazini Mashariki ni jimbo pekee ambalo lilifunga huduma za Mahakama Kuu.
“Hii ni sawa na kufanya jimbo la Kaskazini Mashariki kuhisi kuwa sehemu ya nchi hii na siyo sehemu iliyodharauliwa,” aliiambia Sabahi.
Alisema Mwanasheria Mkuu Willy Mutunga alitarajiwa kutembelea Garissa mwezi Julai kufanya mkutano kwenye jengo la halmashauri ya mji na kutathmini maendeleo ya Mahakama hii.
Mahakama Kuu za jimbo ni Mahakama za juu za tatu za Kenya zenye uwezo wa kusikiliza shauri na kutoa hukumu baada ya Mahakama ya Juu na Mahakama ya Rufaa. Zina mamlaka ya kisheria yenye ukomo katika uhalifu na masuala ya kiraia, lakini zina madaraka ya kusimamia Mahakama zilizo chini yake kama vile mahakama ya Wilaya, Mahakama ya Kadhi na Mahakama ya Kijeshi.
“Yeyote ambaye hajaridhika na hukumu iliyotolewa katika mahakama zilizo chini yake anaweza kukata rufaa katika Mahakama Kuu,” Mutuku alisema. Hadi sasa mahakama hii imesikiliza kesi 20.
Wakazi wa ndani walisema mahakama hii imewarahisishia raia kupata haki.
Abdisalam Ahmed Abdi, mkulima mwenye umri wa miaka 53, aliiambia Sabahi kuwa aliihamisha kesi yake kwenda Mahakama Kuu mwezi uliopita kutafuta hati ya kusitisha utekelezaji na kusubiri hukumu juu ya pendekezo la ardhi linalohusisha ekari zake nane huko Weel Adheey jirani na Garissa.
Halmashauri ya Mji huo ilijumuisha ardhi yake kama sehemu ya mpango wa maendeleo ya mji, alisema. “Nilikwenda mahakamani chini ya hati ya dharura kwa sababu hatua iliyochukuliwa na mji huo imekiuka Sheria ya Amana ya Ardhi na Sheria ya Ufilisi ya Ardhi,” alisema.
“Halmashauri ya Mji huo imenifukuza na kuanza kugawa sehemu yangu ya ardhi kwa maendeleo,” alisema. Abdi alisema bado kesi yake haijasikilizwa, lakini asingekuwa amekwenda Mahakam Kuu, mgawanyo wa ardhi ungeweza kuendelea bila kuzuiliwa.

Kurahisisha usumbufu wa kifedha kwa ajili ya kupata haki

Mohammed Nur Kulow, mwanasheria mwenye kampuni ya Kulow and Company Advocates huko Garissa, alisema wananchi waliotaka kuwasilisha kesi zao awali walitakiwa kusafiri hadi Nairobi, Mombasa au Embu.
"Zaidi ya ada kubwa, wananchi walitakiwa kugharamia usafiri na mahali pa kulala. Kesi hizo mara kwa mara huairishwa kwa sababu mbalimbali, na kurejea na hivyo zilikuwa zikigharimu fedha kwa wananchi wengi ambao ni maskini," aliiambia Sabahi.
Aidha, kufanya huduma iwe ya gharama nafuu kwa kuondoa gharama za usafiri, mahakama mpya itasaidia kuondoa msongamano katika mahakama za majiji mengine makubwa na kuharakisha kesi kwa kila mmoja, alisema Kulow.
Adan Gedi Hujale, mwenye umri wa miaka 36 mmiliki wa duka la majenereta huko Garissa, alisema aliwasilisha kesi yake katika Mahakama Kuu ya Nairobi mwaka 2009 kumpinga mwendelezaji binafsi ambaye aliingia katika ardhi yake ya eka moja huko Ijara.
"Kesi ilichukua miaka miwili kusikilizwa kwa upande wangu, lakini nilitumia zaidi ya shilingi 600,000 (Dola za Kimarekani 7,200). Ada ya mwanasheria ilikuwa chini ya shilingi 200,000 na nyingine nilizitumia kwa ajili ya usafiri, chakula na mahali pa kulala kwa ajili ya mashahidi wangu, mwanasheria wangu na mimi mwenyewe," alisema.
Hujale alisema alitakiwa kuuza mifugo kwa ajili ya kugharamia kesi yake. Kama mahakama ingekuwa karibu angekuwa na uwezo wa kuokoa fedha na mifugo yake, alisema.
Charles Onono, mwanasheria wa huko Garissa, alisema kuwepo kwa Mahakama Kuu kumehimiza pia kufunguliwa kwa asasi mpya za kisheria katika jimbo.
"Kabla ya Mahakama Kuu kuanzishwa, kulikuwa na asasi mbili tu za kisheria katika jimbo – sasa tuna asasi za kisheria zaidi ya tano," alisema. "Zaidi ya kuleta huduma za kisheria karibu na watu, asasi hizo zimesaidia kuongeza ajira."
Khalif Abdi Farah, mratibu wa Northern Forum for Democracy, aliiambia Sabahi kwamba kuanzishwa kwa mahakama ni sehemu ya jitihada zinazoendelea za serikali kurekebisha mahakama, ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya majaji na mahakimu nchini.
Matokeo yake, Kenya iliapa katika kikao chake cha kwanza cha Mahaka ya Juu ya Kisheria mwezi Agosti, 2011, na iliteua majaji wapya 28 wa Mahakama Kuu, alisema Duncan Okello, mkuu wa wafanyakazi katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu.
"Hatua zaidi za marekebisho zitafuata ili kuboresha kiwango, kasi na upatikanaji wa haki," alisema.

No comments:

Post a Comment

KARIBU