Milipuko ya kando ya barabara iliyoulenga msafara wa Kikosi cha Umoja
wa Afrika cha Kulinda Amani nchini Somalia (AMISOM) baina ya Kismayu na
makutano ya Afmadow iliwajeruhi wanajeshi watatu na raia wawili siku ya
Jumatano (tarehe 17 Julai), ilisema AMISOM kwenye taarifa yake kwa
vyombo vya habari.
Waandishi wawili wa habari waliokwenda kuripoti tukio hilo walipigwa
risasi na watu wenye silaha wasiojulikana, liliripoti shirika la habari
la AFP.
Mascud Abdulahi Adan, ripota wa Redio Dalsan, alijeruhiwa vibaya kwa
risasi ya shingo, ambapo Mohamed Farah Sahal, anayefanya kazi na Redio
Goobjoog, alipigwa risasi begani, kwa mujibu wa Chama cha Waandishi wa
Habari cha Somalia.
"Mascud alikuwa akijaribu kuripoti mashambulizi hayo ... na alikuwa
njiani kwenda kwenye tukio pale alipopigwa risasi, alisema mkurugenzi wa
Redio Dalsan, Hassan Ali Gesey.
Haikuwa wazi ikiwa waandishi hao walilengwa wao moja kwa moja.
No comments:
Post a Comment