..

..
.

Saturday, 20 July 2013

Jumuiya ya Afrika Mashariki karibu itakuwa na pasipoti ya pamoja, viza ya utalii

Uamuzi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuridhia viza ya pamoja kwa utalii katika kanda na pasipoti kwa raia wa EAC ifikapo mwishoni mwa 2014 umepokelewa kwa hisia mchanganyiko.
  • Viza moja ya utalii kwa ajili ya kusafiri ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki itawashawishi watalii zaidi kwenye kanda na kuwezesha usafirishaji wa bidhaa, watu na huduma. Picha ya hapo juu, msichana mdogo akiwa amepanda ngamia katika ufukwe wa Bamburi huko Mombasa, Kenya. [Ivan Lieman/AFP]
  • Rais wa Rwanda Paul Kagame (kushoto) akitembea kando ya Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza (katikati) na Rais wa Tanzanian Jakaya Kikwete (kulia) wakati wakiwasili kwenye Mkutano wa kawaida wa 14 wa Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki huko Nairobi tarehe 30 Novemba, 2012. [Tony Karumba /AFP]
Mwezi uliopita wajumbe wa EAC walikutana Arusha, Tanzania, ambapo walikubaliana ratiba mpya kwa utoaji wa pasipoti ya kanda kwa mwaka ujao. Tarehe 6 Julai, mawaziri wa utalii kutoka nchi wanachama wa EAC -- Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda -- walikutana Burundi ambapo waliainisha malengo mapya kwa kurudisha nyuma visa ya utalii ya pamoja hadi ifikapo Julai mwakana. Mawaziri hao pia waliunda kikosi kazi kusimamia utekelezaji wa itifaki ya viza mpya na kutatua masuala yoyote yaliyobakia.
EAC imekuwa ikifanyia kazi pasipoti na viza ya pamoja kutoka 2005, lakini jitihada hizo zimekuwa zikicheleweshwa kutokana na wasiwasi wa usalama, miundombinu dhaifu, na kutokukubaliana juu ya utaratibu wa ada ya viza na mitindo wa kushirikiana mapato, alisema katibu wa baraza la mawaziri la Kenya wa Mambo ya Ndani na Uratibu wa Serikali Kitaifa Joseph Ole Lenku.
"Masuala yote yaliyobakia yataangaliwa na yatatatuliwa kabla ya kufikia tarehe ya mwisho," Lenku alisema. "Hii ndiyo sababu iliyofanya tuahirishe kupitisha viza hiyo, ambayo ilipangwa kutekelezwa mwaka huu, kutoa muda zaidi kwa ajili ya kushughulikia kwa makubaliano tofauti hizo."
Kukidhi tarehe mpya ya mwisho, nchi wanachama zilikubaliana kulinganisha sheria zao za uhamiaji kwenye lengo la EAC na kuweka teknolojia inayohitajika kwa ujumuishaji wa mifumo ya mtandao wa taarifa zao.
"Hili litasaidia kuleta mwafaka kwenye mifumo ya usimamizi wa uhamiaji na kusaidia mtandao pamoja na maeneo ya mpaka na balozi za nchi zote wanachama, Lenku alisema.
Mfumo wa pamoja utatoa fursa kwa EAC kushirikishana taarifa kuhusu watu wanaosafiri katika nchi ndani ya kanda na kuzuia uhalifu kutovuka kutoka nchi moja kwenda nyingine, alisema, akiongezea kwamba makubaliano juu ya taratibu za viza na muundo wa ada vilikuwa vikiendelea.

Pasipoti moja ya EAC

Kuhusiana na pasipoti moja, baraza la Mawaziri la EAC limepanga tarehe 31 Julai kuwa mwisho wa kutoa aina ya waraka wa kusafiria siku zijazo, alisema Nyamajeje Weggoro, mkurugenzi wa sekta za uzalishaji katika EAC.
"Hadi sasa, tulichokubaliana ni kwamba pasipoti itakuwa na rangi za bendera ya EAC, na mwonekano na alama nyingine za kiusalama [zitafuata] viwango vya shirika la kiraia la kimataifa," aliiambia Sabahi.
Ujumbe kutoka EAC pia ulikubaliana kwamba pasipoti hiyo, kama zilivyo pasipoti nyingine zinazotumika katika ukanda huo, itakuwa imepachikwa chipu ndogo ambayo itatunza taarifa binafsi za mtu.
Itakuwa ni kazi ya kila nchi kwa nchi zote tano kuamua iwapo wananchi wake wanatumia pasipoti zote ya taifa na ya EAC, au kutumia pasipoti moja yenye majina yote la EAC na jina la nchi yao, alisema Weggoro.
Nchi wanachama wa EAC kwa sasa zinatoa pasipoti za muda kwa ajili ya kusafiria ndani ya nchi za jumuiya hiyo. Pasipoti hizo, zinatumika zaidi na wanafunzi na wafanyabiashara, zinawaruhusu wamiliki kupata viza binafsi kwa kila nchi za EAC ambazo lazima zitengenezwe upya kila baada ya miezi sita.
"Tumekuwa tukipingana nchi husika kuharakisha uanzishaji wa viza moja ya utalii ili kupata watalii zaidi. Imesubiriwa kwa muda mrefu, lakini angalau sasa tumepata ahadi kutoka kwa nchi wanachama kutimiza hilo," Ofisa mtendaji mkuu wa Shirikisho la Utalii la Kenya Agatha Juma aliiambia Sabahi.
Juma alisema alihamasishwa na uamuzi wa EAC kuunda kikosi kazi kwa ajili ya kushughulikia masuala yote ambayo yalisalia na kuhakikisha kwamba hatua hizo mbili zinatekelezwa kwa kufuata tarehe ya mwisho ya utekelezaji. Shughuli za utalii zinafanyika kwa mabadiliko, ambayo yataongeza utalii na kuwavutia wageni zaidi katika maeneo hayo kwa kurahisisha mambo ya usafiri, alisema.
"Taratibu za viza ambapo watalii wamelazimishwa kuwa na nyaraka nyingi muda wowote wanapopita katika mipaka yetu imekuwa ikipoteza muda na kukatisha tamaa," alisema.
Tozo pia zinapaswa kusaidia kuwashawishi watalii kutoka nchi za ng'ambo, kwa sababu wataweza kusafiri katika Afrika Mashariki nzima kwa kutumia viza moja, alisema Juma.

Kurahisisha vikwazo vya kusafiri katika eneo

Lakini Julius Karanja, mwendeshaji wa shughuli za utalii na Twiga Tours anayeishi Nairobi, ambaye hutoa safari za anasa nchini Kenya na Tanzania, alionyesha wasiwasi kwamba EAC itakamilisha kwa tarehe hiyo iliyopangwa.
"Tumesikia ahadi hizo kabla, na sina uhakika kama zitakamilishwa ili tupate unafuu wa mifumo [hii] ambayo iliamuliwa kuondolewa miaka minne iliyopita wakati mkataba wa umoja wa forodha na soko huria ulipoanzishwa," alisema.
"Vikwazo hivi vya kibiashara ambavyo vinaendelea kufifisha uhusiano, kwa maoni yangu vinaweza kutatuliwa tu kama nchi katika ngazi ya taifa zitaamua kushughulikia, na sio kupitia mikutano ya kanda ambayo viongozi wa ngazi za juu wanakutana na kuahidi mambo," alisema Karanja.
Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki Vimal Shah alionyesha matumaini zaidi, akisema kwamba pasipoti moja itaongeza biashara za eneo hilo na  
"Pamoja na utekelezaji wake, Watu wa Afrika Mashariki watachukuliwa kama wamoja. Sitahitaji kutafuta kibali cha kufanya kazi ili kupata kazi nchini Uganda wakati mimi ni Mkenya," alisema Shah. "Hili litaruhusu uingiaji huru wa wafanyakazi katika eneo letu hivyo kuimarisha muingiliano."
Alisema pasipoti moja ingesaidia kupunguza gharama ya kufanya biashara katika Afrika Mashariki.
Wakati huo huo, Mark Omolo, mwanafunzi wa uchumi kutoka Kenya aliyejiandikishwa katika Chuo Kikuu cha Makerere huko Kampala, Uganda, alisema pasipoti ya EAC itaokoa shilingi 8,000 (Dola 92) zake za kila baada ya miezi sita na usumbufu za kutengeneza upya nyaraka zake.
"Limekuwa jambo gumu kwa wanafunzi [kwa sababu] kila baada ya miezi sita tunatakiwa kusafiri kwenda kwenye vituo vya mpaka kuhuisha kuendelea kwetu kubakia Uganda, lakini tuna imani mpango huu utasaidia kuokoa fedha, utatufanya tuhisi [sisi ni] wamoja kama Afrika Mashariki na [kusaidia watu] kuingiliana kwa urahisi," aliiambia Sabahi.

No comments:

Post a Comment

KARIBU