Kuna habari za kutia wasi wasi kwamba baadhi ya wakulima nchini Tanzania
wanatumia vumbi la madini ya uraniumu ili kuhifadhia mazao yao kama
vile nafaka na matunda. Kwa mujibu wa mbunge wa Ujerumani Ute Koczy .
Mbunge huyo wa chama cha kijani nchini Ujerumani Ute Koczy
ametahadharisha kwamba matumizi ya vumbi la madini ya Uranium kwa ajili
ya kuhifadhia mazao ya kilimo yanaweza kusababisha hatari kubwa kwa
wakulima.
Kutokana na hatari kubwa iliyopo mbunge huyo amesema pana haja kwa
serikali ya Tanzania kuchukua hatua, angalau kwa ,kutoa habari kwa
ukamilifu, "Sisi tunaona pana umuhimu mkubwa kwa serikali ya Tanzania na
taasisi mbalimbali kulishughulikia suala hilo.Serikali na taasisi
zinapaswa kutoa habari kwa ukamilifu ili watu wajue ni nini kinaweza
kutumika na nini kinapaswa kuachwa."
Kwa muda wa miaka mingi mbunge huyo wa Ujerumani Ute Koczy ambae ni
msemaji wa wabunge wa chama cha kijani juu ya masuala ya maendeleo
amekuwa anafuatilia kwa undani shughuli zinazohusu uzalishaji wa madini
ya uranium nchini Tanzania. Na hivi karibuni alikuwaa nchini Tanzania
ambako aliweza kuijionea mwenyewe shughuli zinazohusu uzalishaji wa
madini ya uranium . Kutokana na hatari ya vumbi la madini hayo
linalotumiwa na baadhi ya wakulima nchini Tanzania, mbunge huyo
ameandika barua kwa Shirika la kudhibiti matumizi ya nishati ya nyuklia,
na pia kwa Rais na Waziri Mkuu wa Tanzania. Jee ni nini hasa anata
katika barua alizoandika? "Nionavyo mimi pana mambo ya kichini chini
yanayotokea. Tunaingiwa wasiwasi tunaposikia kwamba wakulima nchini
Tanzania wanaanza kutumia vumbi la madini ya uranium ili kuhifadhia
mazao yao.Sasa tunaanza kujiuliza jee kinatokea nini nchini Tanzania?
alisema mbunge huyo.
Mbunge huyo wa Ujerumani bibi Ute Koczy aliongeza kusema ni hatari kubwa
kwa wakulima na kwa watu wengine nchini Tanzania kukaribiana na vumbi
la madini ya uranium.
Aidha alisema mpaka sasa hakuna data na takwimu zinazofahamika juu ya
viwango vya miali inayoweza kuwa hatari.Kuna habari zinazopingana juu ya
hayo. Kutokana hali iliyopo mbunge huyo anataka kupigwa marufuku kabisa
kwa matumizi ya vumbi la uranium nchini Tanzania.
Hata hivyo ni vigumu kwa mbunge huyo kusema ni kiasi gani cha vumbi la
uranium kinachohusika kwa jumla. Lakini amesema mashirika yasiyo ya
kiserikali yameteoa tahadhari na shirika la nishati ya kiatomiki la
Tanzania pia limethibitisha habari hizo.
No comments:
Post a Comment