Akizungumza na waandishi wa habari
Dar es salaam jana, Ofisa Masoko wa Kampuni hiyo, Jaqulini Nnunuma
alisema Tanzania ina idadi kubwa ya watu ambao wanatumia simu za
mikononi na asilimia 50 ni wateja wa tigo, hivyo wameamua kuanzisha
vifaa vya nishati ya jua vyenye uwezo wa kuchaji simu kwa lengo la
kurahisisha huduma zao.
ILI kuwaongezea wateja wake uwanja mpana wa
kutumia mawasiliano ya simu, Kampuni ya simu za Mkononi ya Tigo,
imezindua kifaa maalum cha kuchaji simu kinachotumia nishati ya jua.
Kifaa
hicho kitawafanya wananchi hasa wanaoishi vijijini ambako hakuna
nishati ya umeme kuweza kuchaji simu zao, hivyo kuongeza idadi ya
watumiaji wa mawasiliano ya simu nchini.
Akizungumza na waandishi
wa habari Dar es salaam jana, Ofisa Masoko wa Kampuni hiyo, Jaqulini
Nnunuma alisema Tanzania ina idadi kubwa ya watu ambao wanatumia simu
za mikononi na asilimia 50 ni wateja wa tigo, hivyo wameamua kuanzisha
vifaa vya nishati ya jua vyenye uwezo wa kuchaji simu kwa lengo la
kurahisisha huduma zao.
‘’Tanzania ina idadi kubwa ya watu ambao
hawana njia ya moja kwa moja ya kupata umeme, hivyo leo tumeamua
kuzindua rasmi kifaa maalum cha nishati ya jua kwa ajili ya kuchaji simu
za mikononi’’alisema Nnunduma.
Pia aliongeza kuwa pamoja na
kuwapa wateja nishati rafiki na endelevu kwa matumizi ya kila siku,
watakaonufaika na mradi huu ni wale wanaoendesha maisha na biashara zao
katika maeneo yasiyo na umeme .
‘’Kwa kuwapa wateja wetu nishati
rafiki na endelevu kwa matumizi ya kila siku watakaonufaika na mradi
huu ni wale wale wanaoishi na kuendesha biashara zao katika maeneo
yasiyo na umeme tu’’ aliongeza Nnunduma.
Naye Meneja Miradi ,
Yaya Ndoje alisema kuwa watakaonufaika na huduma hiyo endelevu kwa
ajili ya kutoa huduma hiyo ya kusambaza vifaa hivyo ni wale walio
mawakala wa tigo tu, pamoja na wauzaji wa bidhaa za tigo kama simu na
chaji pekee katika mikoa yote nchini Tanzania Bara na Visiwani.
Aidha
aliongeza kuwa kwa kupitia vifaa vya nishati ya jua huduma hii bunifu
itarahisisha na kufanya na upatikanaji wa huduma ya tigo iwe rahisi
pamoja na kuongeza kipato ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma kwa
kipindi kwa wateja wetu.
No comments:
Post a Comment