MTUHUMIWA NA MGONJWA WANAINGIZWA KATIKA GARI LA MWESHIMIWA DIWANI TAYARI KWA KUPELEKWA POLISI
Katika hali isiyo ya Kawaida Mkazi wa majengo
jijini Mbeya Ndugu Bahati Rukangara amemchoma moto mtoto mdogo wa mika 3
aliyefahamika kwa jina la Aneth kisha kumfungia Ndani na kumlazimisha ale
kinyessi chake.
Akizungumza Mwenyekiti wa mtaa huo Ndugu
Habiba Mwakitabu amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya
saa 10 :30 asabuhi ambapo majirani na mwanamke huyo waligundua mara baada ya
kusikia sauti ya mtoto huyo akilia kutokana na maumivu.
Amesema mara baada ya kusikia sauti hiyo walifika
eno hilo na kunza kumhoji ili kufahamu kiini cha tatizo hilo ambapo
alishindwa kutoa ushirikiano ndipo walipo anza kumpiga .
Amesema kutokana na hali hiyo majirani
walilazimika kubomoa mlango ndipo walipo mkuta mtoto huyo akiwa uchi huku
ameungua vibaya mwilini hasa katika upande mmoja eneo la mkono wa kushoto .
Amesema mara baada ya kumhoji mtoto huyo
aliwaeleza kuwa mama yake mdogo alichukua nguo na mkumfunga mkononi kisha
kumwagia maji ya moto pamoja na kumlazimisha ale kinyesi chake hali ambayo
iliwafanya washindwe kuvumilia na kuanza kupiga kelele kwa lengo la kuomba
msaada kwa watu wengine.
Kwa mujibu maelezo ya mwenyekiti huyo amesema
kuwa Mtuhumiwa huyo amekuwa akifanya vitendo vya manyanyaso kwa mtoto huyo
marakwamara ambapo wamekuwa wakimuonya lakini amekuwa si mtu wa kusikia.
Ameesema mtoto huyo si wa kwa kwakwe kwani
amekuwa akiishi naye kwa muda mrefu sasa ambapo aliachiwa na dada yake ambaye
hakufahamika kuwa nayishi wapi kwa sasa.
Hata Diwani wa kata hiyo Ndugu Samuel Mamboma
alifika eneo hilo tukio na kutoa msaada wa usafiri kwa lengo la kumfikisha mama
huyo polisi pamoja na mtoto huyo ambaye naye alikimbizwa Hospitali.
Hata hivyo amesema tukio hilo si la kwanza
kutokea katika meaeno hayo kwani kumekuwepo na matukio mengi hasa ya utoaji
mimba na kutupwa watoto.
No comments:
Post a Comment