ONA JINSI MASHABIKI WA COASTAL UNION NA YANGA WANAVYOCHIMBIANA MKWARA JIJINI TANGA LEO... WAKATIZA MITAANI JIJINI TANGA KWA TAMBO NA VIJEMBE ... VIINGILIO MECHI YAO KWENYE UWANJA WA MKWAKWANI VYAANDIKA REKODI... WATU WAANZA KUFURIKA UWANJANI KUANZIA SAA 7:00 MCHANA....!
Mashabiki wa Yanga wakiandamana na vigoma na vuvuzela katikam maeneo ya stendi kuu ya mabasi jijini Tanga leo ikiwa ni mikwara yao kabla ya kuwavaa Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani jioni. |
Mechi kali ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara itakayokuwa ya kumalizia mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo kati ya wenyeji Coastal Union na Yanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo jioni imeandika rekodi baad ya tiketi zake kuuzwa kwa bei 'mbaya' kuliko mechi zote za msimu huu ikiwamo ya mabingwa watetezi, Simba dhidi ya wenyeji hao (Coastal).
Mauzo ya tiketi hizo leo ni Sh. 5,000 kwa kiingilio cha chini (ambazo kufikia saa 9:00 watu walikuwa wakizilangua kwa Sh. 7,000), Sh. 10,000 na Sh. 15,000 kwa kiingilio cha juu wakati katika mechi nyingine zenye mvuto zaidi ikiwamo ya Simba dhidi ya Coastal, viingilio vilikuwa Sh. 4,000, Sh. 7,000 na Sh. 10,000.
Licha ya viingilio hivyo vikubwa, mashabiki walionekana wakichangamkia tiketi hizo kwa wingi, wengine wakitokea jijini Dar es Salaam na baadhi katika maeneo ya jirani ya jiji la Tanga kama Kabuku, Mwakidila, Duga Maforoni, Pangani, Muheza, Korogwe na kwingineko
No comments:
Post a Comment