Mkutano huo unafanyika huku viongozi wakikabiliwa na shinikizo la
kuepukana na makosa yaliyofanywa awali, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa
barabara kubwa kubwa ambazo hazina magari mengi, viwanja vya ndege
ambavyo ni nadra kutumiwa kwa usafiri wa ndege na reli za treni za
kwenda kasi zinazobeba abiria wachache. Viongozi wanakabiliwa na
changamoto ya kulipa fedha zilizotumika katika miradi hiyo.
Kunatarajiwa kuwa na kibarua kigumu kufikia makubaliano ya bajeti ya Umoja wa Ulaya ya mwaka 2014-2020 katika mkutano huo. Changamoto nyingine kubwa itakuwa kujiepusha na majaribu ya kutenga mabilioni ya euro kwa ajili ya miradi ambayo baadaye inakuwa ni kumbukumbu ya hasara tupu.
Tofauti kubwa ya maoni
Nchi kadhaa zimeapa kutumia kura yao ya veto kukwamisha bajeti iliyopendekezwa. Nchi zinazochangia kiwango kikubwa cha fedha zinataka bajeti hiyo ipunguzwe kufikia bilioni 100 zikisema haiingii akilini kuongeza matumizi katika Umoja wa Ulaya wakati nchi za Ulaya zikifunga mkaja.
Ujerumani inaamini kushindwa kwa viongozi wa Ulaya kukamilisha bajeti hiyo halitakuwa jambo kubwa la kutia wasiwasi. Duru za serikali ya Ujerumani zinasema bado kuna muda na kwamba kama miezi kadhaa itahitajika ili kutolewe maoni na uratibu wa kisiasa ufanyike katika miji mikuu ya Ulaya, basi hautakuwa mwisho wa dunia.
Fedha za Umoja wa Ulaya zimeleta manufaa makubwa kwa watu masikini katika mataifa ambayo hayajaendelea sana Ulaya na kwingineko duniani. Kwa mfano zimesifiwa kwa kuisadia Poland kuepuka kutumbukia katika mdororo wa kiuchumi wakati wa mgogoro wa sasa wa uchumi na kwa kuyaokoa maisha ya wengi kupitia misaada ya kigeni na kusaidia utafiti wa kitabibu.
Viongozi kumwaga cheche
Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, leo ameapa kupigania bajeti itakayodhihirisha hatua za kubana matumizi zinazofanywa kitaifa kwa masilahi ya walipa kodi wa Uingereza na Ulaya nzima kwa ujumla.
Kwa upande mwingine, waziri mkuu wa Ubelgiji, Elio Di Rupo, ameonya leo kwamba kupunguza kwa kiwango kikubwa matumizi katika Umoja wa Ulaya litakuwa kosa kubwa. Amewaambia waandishi wa habari alipowasili mjini Brussels kuwa, "Lazima tuwe na bajeti yenye malengo makubwa. Kwa sasa tunahitaji uwezo wa kifedha kuliko wakati mwingine wowote, ili tuweze kusambaza upya, tuwe na sera mpya - yaani sera za viwanda."
Di Rupo amesema atapigania fedha za kutosha kwa ajili ya kilimo na maeneo masikini kabisa ya Ulaya, ikiwa ni pamoja na jimbo la nchi yake la Limburg, ambalo lilipatwa na mshangao mkubwa mwezi uliopita kwa taarifa za kufungwa kiwanda cha kutengeneza magari cha kampuni ya Ford. Hakuondoa uwezekano wa kutumia kura ya turufu ikihitajika.
Mwandishi: Hasselbach, Christoph/Josephat Charo
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman
Kunatarajiwa kuwa na kibarua kigumu kufikia makubaliano ya bajeti ya Umoja wa Ulaya ya mwaka 2014-2020 katika mkutano huo. Changamoto nyingine kubwa itakuwa kujiepusha na majaribu ya kutenga mabilioni ya euro kwa ajili ya miradi ambayo baadaye inakuwa ni kumbukumbu ya hasara tupu.
Eneo la mkutano Brussels
Fedha zinazotumika kwa ajili ya ujenzi wa barabara, daraja na
miundombinu mingine katika maeneo masikini kabisa ya Umoja wa Ulaya
zinajumuisha asilimia 33 ya bajeti ya thamani ya euro trilioni 1 kwa
kipindi cha miaka saba ijayo. Kiwango hiki kinakariba fedha zilizotengwa
kwa ajili ya kilimo.Tofauti kubwa ya maoni
Nchi kadhaa zimeapa kutumia kura yao ya veto kukwamisha bajeti iliyopendekezwa. Nchi zinazochangia kiwango kikubwa cha fedha zinataka bajeti hiyo ipunguzwe kufikia bilioni 100 zikisema haiingii akilini kuongeza matumizi katika Umoja wa Ulaya wakati nchi za Ulaya zikifunga mkaja.
Ujerumani inaamini kushindwa kwa viongozi wa Ulaya kukamilisha bajeti hiyo halitakuwa jambo kubwa la kutia wasiwasi. Duru za serikali ya Ujerumani zinasema bado kuna muda na kwamba kama miezi kadhaa itahitajika ili kutolewe maoni na uratibu wa kisiasa ufanyike katika miji mikuu ya Ulaya, basi hautakuwa mwisho wa dunia.
Jean-Claude Juncker
Waziri mkuu wa Luxembourg, Jean-Claude Juncker, ambaye anaongoza jopo
la mawaziri wa fedha wa kundi la nchi zinazotumia sarafu ya Euro,
ameonya kuhusu mazungumzo magumu katika mkutano wa kilele wa Umoja wa
Ulaya mjini Brussels. Juncker amesema misimamo inatofautiana mno na
haitokuwa rahisi kufikia mapatano kwa haraka.Fedha za Umoja wa Ulaya zimeleta manufaa makubwa kwa watu masikini katika mataifa ambayo hayajaendelea sana Ulaya na kwingineko duniani. Kwa mfano zimesifiwa kwa kuisadia Poland kuepuka kutumbukia katika mdororo wa kiuchumi wakati wa mgogoro wa sasa wa uchumi na kwa kuyaokoa maisha ya wengi kupitia misaada ya kigeni na kusaidia utafiti wa kitabibu.
Viongozi kumwaga cheche
Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, leo ameapa kupigania bajeti itakayodhihirisha hatua za kubana matumizi zinazofanywa kitaifa kwa masilahi ya walipa kodi wa Uingereza na Ulaya nzima kwa ujumla.
Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron
Akizungumza muda mfupi baada ya kuwasili Brussels, Cameron amesema
haridhiki kabisa na pendekezo la bajeti wakati huu wanapopitisha maamuzi
magumu kuhusu matumizi ya fedha za umma. Amesema litakuwa kosa kubwa
kuwepo na pendekezo la kuongeza matumizi katika bajeti ya Ulaya.Kwa upande mwingine, waziri mkuu wa Ubelgiji, Elio Di Rupo, ameonya leo kwamba kupunguza kwa kiwango kikubwa matumizi katika Umoja wa Ulaya litakuwa kosa kubwa. Amewaambia waandishi wa habari alipowasili mjini Brussels kuwa, "Lazima tuwe na bajeti yenye malengo makubwa. Kwa sasa tunahitaji uwezo wa kifedha kuliko wakati mwingine wowote, ili tuweze kusambaza upya, tuwe na sera mpya - yaani sera za viwanda."
Di Rupo amesema atapigania fedha za kutosha kwa ajili ya kilimo na maeneo masikini kabisa ya Ulaya, ikiwa ni pamoja na jimbo la nchi yake la Limburg, ambalo lilipatwa na mshangao mkubwa mwezi uliopita kwa taarifa za kufungwa kiwanda cha kutengeneza magari cha kampuni ya Ford. Hakuondoa uwezekano wa kutumia kura ya turufu ikihitajika.
Mwandishi: Hasselbach, Christoph/Josephat Charo
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman
No comments:
Post a Comment