..

..
.

Thursday 22 November 2012

Mapambano yasimamishwa Gaza

Palestinians celebrate what they say is a victory over Israel after an eight-day conflict in Gaza City November 21, 2012. Israel and the Islamist Hamas movement ruling the Gaza Strip agreed on Wednesday to an Egyptian-sponsored ceasefire to halt an eight-day conflict that killed 162 Palestinians and five Israelis. REUTERS/Ahmed Zakot (GAZA - Tags: CONFLICT POLITICS) 
 Baada ya mapigano ya siku nane Israel na wapiganaji wa Hamas wamekubaliana kuziweka silaha chini. Pande mbili hizo ziliyasimamisha mapigano kuanzia saa moja ya usiku hapo jana
Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na Waziri wa Ulinzi Ehud Barak
  Makubaliano hayo yalifikiwa kwa upatinishi wa Misri. Hatua hiyo ilitangazwa mjini Cairo na Waziri wa mambo ya nje wa Misri Kamel Amr kwenye mkutano na waandishi wa habari ambapo Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton pia alikuwapo.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepongeza hatua hiyo ya kusimamisha mapigano. Katika tamko lake Baraza hilo la wanachama 15 limesema limesikitishwa juu ya vifo vya watu na limetoa mwito wa kuhakikisha usalama wa raia na kuwalinda kwa mujibu wa sheria za kimataifa.
Baraza hilo pia limezitaka pande mbili za mgogoro ziitekeleze hatua hiyo ya kusimamisha mapigano. Limepongeza juhudi za Rais wa Misri Mohamed Mursi katika kuleta amani. Pia limempongeza Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kwa juhudi zake wakati wa ziara yake katika Mashariki ya Kati
Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na Waziri wa Ulinzi Ehud Barak
Mapatano hayo yamekomesha siku nane za mauaji kwenye Ukanda wa Gaza na kusini mwa Israel. Wapalestina zaidi ya 150 na Waisraeli watano waliuawa. Miundo mbinu kadhaa pia iliteketezwa. Wapiganaji wa Hamas waliishambulia Israel kwa mamia ya roketi hadi mji wa Tel-Aviv na majeshi ya Israel yaliushambulia Ukanda wa Gaza kwa ndege.
Kiongozi wa Hamas Khaled Meshaal ameiunga mkono hatua ya kusimamisha mapigano na ameielezea kuwa ni kushindwa kwa Israel. Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema amekubali kutoa fursa ya kuleta amani, lakini wakati huo huo ameonya kwamba atakuwa tayari kuchukua hatua kali za kijeshi ikiwa itakuwa lazima.Muda mfupi kabla ya kufikiwa mapatano ya kusimamisha vita, majeshi ya Israel na wapiganaji wa Hamas waliendelea kushambuliana.
Hapo jana bomu liliripuka ndani ya basi katika mji wa Tel-Aviv. Watu wasiopungua 15 walijeruhiwa na watatu miongoni mwao vibaya sana. Hatua ya kusimamisha mapigano ilipokewa kwa furaha kubwa kwenye Ukanda wa Gaza.Risasi na fataki zilifyatuliwa hewani katika mji wote wa Gaza City huku mamia kwa mamia ya watu wakijitokeza barabarani kusherehekea.
Mwandishi: Mtullya Abdu/afp,Reuters,dpa,AP
Mhariri: Abdul-Rahman

No comments:

Post a Comment

KARIBU