..

..
.

Monday, 22 October 2012

WATUHUMIWA WA UCHOMAJI MAKANISA MBAGALA WAPANDISHWA KIZIMBANI TENA




WATUHUMIWA wa kuharibu na kuchoma moto makanisa huko Mbagala jijini Dar es Salaam, mapema leo wamefikishwa mbele ya Hakimu Binge Mashabala wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. 
Watuhumiwa hao watano wamesomewa mashtaka matano na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka, yanayowahusisha na njama za kutenda makosa, kuvunja majengo, uharibifu na wizi wa vifaa vya makanisa na kusabisha hasara ya milioni 550/=. 
Washitakiwa hao, Shabani Hamisi, Issa Abdullah, Kambi Haji, Hamadi Mahambo na Wajabali Julius, walikana makosa hayo na kesi kuahirishwa hadi Oktoba 30 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

KARIBU