..

..
.

Monday 22 October 2012

FILAMU YA KENYA ITASHINDANIA UTEUZI WA TUZO YA ACADEMY


Kuwasilishwa hivi karibuni kwa filamu ya Kenya kwenye Tuzo ya Academy kutafungua njia kwa sekta ya filamu ya nchi kwa watazamaji wa kimataifa na kutoa msukumo unaohitajika sana wa utamaduni wa filamu kwa eneo hili, waangalizi wasema.
  • Picha ya mgando ya filamu ya "Nairobi Half Life" ikionekana wa mwigizaji Joseph Wairimu. [File]
  • Mkurugenzi wa filamu ya "Nairobi Half Life" Tosh Gitonga akizungumza na mashabiki baada ya kuoneshwa kwa filamu hiyo huko Nairobi tarehe 30 Agosti katika Westgate Shopping Mall. [Picha ya Jalada]
"Nairobi Half Life", iliyotengenezwa kwa pamoja baina ya Kenya na Ujerumani, ni moja ya filamu 71 zilizosajiliwa rasmi kushindana kwa ajili ya kuteuliwa filamu tano kwa Tuzo ya Academy cha Sanaa na Sayansi ya Picha za Filamu (Oscars) kwa mwaka 2013, kwa ajili ya kiwango cha Filamu Bora ya Lugha ya Kigeni. Nchi za Afrika ya Kusini, Algeria na Morocco ndio nyengine pekee za Afrika zinazoshindana katika zawadi hiyo.


Filamu hiyo inaelezea maisha ya kijana wa Kenya anayehama kutoka kijijini na kuhamia mjini kwa matumaini ya maisha mazuri, lakini anaishia katika maisha ya uhalifu ili aweze kuishi.
"Hadithi hii NI mbali sana na hadithi za kawaida zinazosemwa kuhusu Afrika. Inatupatia nafasi ya kuhadithia hadithi yetu," mwongozaji wa filamu Tosh Gitonga aliiambia Sabahi.
Alisema kuwa watu kimataifa wanaoangalia filamu wamezoea kuiona Afrika kama ardhi ya njaa tu, lakini kwa filamu hii wataweza kuona ukweli mkubwa zaidi wa miji ya Kiafrika, ambayo inayofanana na yale yanayotokea katika miji duniani kote.
Kwa mujibu wa Nathan Asiago, mkuu wa vipindi katika Tume ya Filamu ya Kenya, kuingizwa kwa filamu hiyo katika orodha ya ushindani kutainua sekta ya filamu ya Kenya.
"Kenya imekuwa na utamaduni usiokuwa wa kawaida -- kumbi za filamu zimekuwa zikihamwa na wenyeji na kuachiwa watalii," alisema, na kuongeza kuwa ushindani unaweza kuibadilisha hali hiyo. "Kama filamu hiyo itashinda au la, mwangaza wa kimataifa utaamsha utamaduni wa kuangalia filamu nchini."
Kushiriki katika Oscars kutazidisha uonekanaji wa sekta ya filamu ya Kenya na kuwavutia wawekezaji na watalii katika eneo hili, lakini pia itasaidia kufufua hamu ya kuangalia filamu zinazofanywa nyumbani, Asiago aliiambia Sabahi.
Kupelekwa kwa filamu hiyo kutatoa fursa kwa watengenezaji filamu wa Kenya kuwasiliana na watoaji filamu wa kimataifa, kuleta nyumbani stadi zaidi na elimu ambayo italea na kukuza sekta ya filamu, alisema.
Mwezi wa Julai, "Nairobi Half Life" ilizawadiwa katika Sherehe za Kimataifa za Maonesho ya Filamu ya Durban nchini Afrika ya Kusini ambapo mwigizaji mkuu Joseph Wairimu alishinda kama Mwigizaji Bora.
Filamu hiyo imezaa hamu nyingi sana katika mzingo wa filamu na ilianza kuoneshwa kwenye filamu za kimataifa hapo tarehe 11 Oktoba huko Kino Koki, Lubeck, Ujerumani na kuoneshwa zaidi kutafanywa katika miji ya Ujerumani ya Hamburg, Bonn, Koln na miji mengine ya Ujerumani kabla ya kumaliza tarehe 26 Oktoba katika Passage huko Leipzig.
Filamu pia itaoneshwa katika majumba ya filamu ya Nairobi ya Planet Media Cinemas Westgate na Century Cinemax Junction kuanzia tarehe 19 hadi 25 Oktoba.
Hapo mwezi wa Novemba, filamu hiyo itakuwa sehemu ya "mafanikio mapya" ya Taasisi ya Filamu ya Marekani katika AFI FEST huko Los Angeles, California kuanzia tarehe 1 hadi 8 Novemba.
Wairimu aliiambia Sabahi anatarajia kuwa kuingia kwa filamu katika Chuo cha Tuzo za Filamu kutahamasisha hamu miongoni mwa waigizaji vijana na kuipa nguvu sekta ya ndani ya filamu. "Kuonekana kwetu huku ni kuzuri, Nina matumaini kuwa filamu yetu itawafanya watu wote hapa kuuona uigizaji kuwa ni taaluma kama zilivyo taaluma nyengine ambazo zinastahiki kuheshimiwa," alisema.
Muigizaji Maina Olwenya, ambaye aliigiza katika sehemu ya filamu hiyo, alisema kuwa ana matumaini kuwa kuingia katika uwanja wa kimataifa kutatangaza kipaji cha Kenya kwenye jukwaa la dunia na kufungua fursa kwa nchi za nje.
Filamu hiyo ni utengenezaji wa pamoja baina ya Ginger Ink Films ya Kenya, One Fine Day ya Ujerumani na DW Akademie inayofadhiliwa na serikali ya Ujerumani.
Hii ni mara ya pili kwa Kenya kuingia katika mashindano. "Heart of Fire" (Moyo wa Moto), ambayo pia ilitengenezwa na Kenya na Ujerumani, iliingia katika kinyang'anyiro cha Filamu Bora ya Lugha ya Kigeni mwaka 2008. Haikupata kuteuliwa.
Uteuzi utatangazwa tarehe 10 Januari, na uwasilishaji wa mwisho wa zawadi kufanyika katika sherehe huko Hollywood, California tarehe 24 Februari.

No comments:

Post a Comment

KARIBU