Kutokana
na kuendelea kwa mfululizo wa matukio mbalimbali yanayosababishwa na
vurugu za kisiasa kati ya baadhi ya vyama vya siasa dhidi ya jeshi la
polisi, ofisi ya msajili wa vyama vya siasa Tanzania imesema imechoshwa
na matukio hayo ambayo yamekua yakisababisha vifo vya mara kwa mara
kwa raia wasio na hatia.
Msajili
wa vyama vya siasa John Tendwa amesema ofisi yake kuanzia sasa
imepanga kuchukua hatua kali za kisheria ikiwemo kukifuta chama
chochote cha siasa kitakachothibitika kufanya mkutano kinyume cha
sheria na kusababisha vurugu pasipo kujali kama vurugu hizo zimedhuru
au hazijadhuru raia yeyote.
Vilevile Tendwa amekemea kampeni mbalimbali zinazoendelea kufanywa nchi nzima na baadhi ya vyama vya siasa na kupewa jina la ‘OPARESHENI’
ambapo amedai kuwa huu si wakati wa vyama kuanza kampeni, hivyo chama
chochote kitakachoendelea na kampeni kwa mtindo huo kuanzia sasa
kitachukuliwa hatua kali ikiwemo kukifutia usajili.
No comments:
Post a Comment