..

..
.

Sunday, September 23, 2012

MFANYABIASHARA AUAWA KIKATILI

MFANYABIASHARA MAARUFU KUTOKA MKOANI KIGOMA LAMECK JONATHAN
''BANDIKO''AMEUAWA KIKATILI KATIKA ENEO LA CHUDA RELINI JIJINI TANGA
NA WATU AMBAO HADI SASA BADO KUFAHAMIKA.

MWILI WA BANDIKO ULIKUTWA UKIWA UMEANZA KUHARIBIKA BAADA YA KUKAA KWA
SIKU MBILI BILA KUTAMBULIWA HADI WALIPOPITA WASAMARIA WEMA AMBAO
WALIKWENDA KUTOA TAARIFA POLISI NA KUSABABISHA WATUMISHI WA IDARA YA
AFYA KUTOKA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA KWENDA KUUCHUKUA NA KWENDA
KUUZIKA KATIKA MAKABURI YA JUMUIYA.

AKIZUNGUMZA KATIKA ENEO LA TUKIO KATIBU WA HAKI ZA BINADAMU MKOANI
TANGA BWANA JONATHAN MWABEJA AMESEMA ONGEZEKO LA WATU KUUAWA KIKATILI
KATIKA KIPINDI CHA WIKI MOJA NI YA KUSIKITISHA HIVYO AMELIOMBA JESHI
LA POLISI KUFANYA KAZI YA ZIADA KUTAFUTA MTANDAO WA WATU WA AINA HIYO
ILI SHERIA IWEZE KUCHUKUA MKONDO WAKE cue in jonathan mwabeja katibu
haki za binadamu Tanga,George leonard mikanjuni sekondari

KUFUATIA TUKIO HILO BAADHI YA WAKAZI WA JIJI LA TANGA WAMESHAURIWA
KUTOA TAARIFA KWA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI PALE WANAPOJIWA NA MGENI ILI
INAPOTOKEA DHARURA HABARI ZIWEZE KUWAFIKIA WALENGWA MUDA MUAFAKA KWA
LENGO LA KUWAKAMATA WATUHUMIWA

No comments:

Post a Comment

KARIBU