..

..
.

Sunday, August 26, 2012

LEMA AJITOSA KUWANIA WAZAZI CCM

 Na Benedict Kaguo
  VUGUVUGU la uchaguzi ndani ya CCM limezidi kushika kasi ambapo wanachama wa Chama chicho wameanza mbio za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho kikongwe hapa nchini.

Uchaguzi huo unatafsiriwa na wachambuzi wengi wa siasa kuwa ndio dira ya chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ambapo CCM na vyama vingine vitasimamisha wagombea katika uchaguzi huo

Kwa kutambua ukweli juu ya Demokrasia kubwa iliyoko ndani ya CCM ambayo inampa nafasi kila mwanachama kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya Chama tayari wanachama mbalimbali wameshaanza mbio za kugombea nyadhifa mbalimbali ndani ya chama hicho.

Tayari Mfanyabiashara Maarufu nchini Bw John Lema ameonesha dhamira ya dhati ya kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ya CCM jumuiya ambayo ndio mlezi wa Chama hicho kutokana na ukweli kuwa imekuwa mstari wa mbele kuzilea jumuiya nyingine za Chama hicho.

Bw Lema ambaye mbali na kuwa Mfanyabiashara maarufu pia hadi anawania nafasi hiyo alikuwa ni  Mlezi wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama hicho Mkoa wa Mwanza ambapo kwa kipindi kirefu amekuwa akikitumikia Chana hicho katika nyanya mbalimbali za maendeleo ambapo baada ya uzoefu wa kutosha kutoka nafasi mbalimbali alizokuwa ameshikilia ndicho kilichomsukuma kutangaza kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Taifa.

Hata hivyo katika chaguzi mbalimbali kumekuwepo na masuala ya Rushwa huku baadhi ya wagombea wakionesha kutumia fedha nyingi kupata madaraka katika eneo hili Bw Lema anamtazamo gani nalo.

Akizungumza mjini Dodoma Bw Lema alionya juu ya wagombea wanaotaka madaraka kwa kutumia fedha na kueleza wazi kuwa hawafai kupewa uongozi kwani pindi watakapopata nafasi hizo watasahau kukitumikia Chama badala yake wataangalia zaidi kujiineemesha wao wenyewe.Anasema wanachama wa CCM wanapaswa kuwaogopa wanaowania uongozi kwa kutumia fedha kwani wakishapata nafasi hizo watashindwa kuwatumia wananchi,na kwenda kutafuta maslahi yao binafsi na hivyo kuifanya Jumuiya hiyo kuendelea kuzorota kimaendeleo licha ya kuwa fursa ya kujiendeleza kichumi.

Anasema uamuzi wa kugombea nafasi hiyo ya Uenyekiti wa Jumuiya hiyo Taifa unatokana na rekodi aliyonayo katika kukitumikia Chama hicho tangu ngazi ya Chikupikizi,Vijana hadi Jumuiya hiyo na kueleza kuwa malengo lukuki ya kuindeleza Jumuiya hiyo kiuchumi ikiwemo kutumia rasilimali zilizopo .

Anasema Jumuiya hiyo ya Wazazi Taifa inapaswa kupata viongozi wasiotanguliza maslahi yao badala yake wapewe nafasi wenye kutanguliza maslahi ya Chama hicho ili kuwezesha mipango ikiwemo ya kuendeleza rasilimali za jumuiya hiyo kufanikiwa.

Anasema pindi atakapochaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya hiyo  atasimamia miradi ya Chama hicho ambayo kwa muda mrefu ilikuwa imedumaa na kuifanya Jumuiya hiyo kukosa mapato ya kutosha ya kuendeshea mipango yake.

“Mfano jumuiya ina kiwanja shekilango Dar es Salaam,tunaweza kujenga hoteli ya nyota tano na kuweka na kumbi za mikutano itachangia kuleta mapato ndani ya chama na jumuiya na fedha tunazo kutokana na uzoefu nilionao katika biashara kuweza kukopa fedha benki kujenga hoteli hiyo,fedha zitatumika kujenga chama na kurudisha deni la benki… tutaanzisha kitengo cha kulea vijana kwa kuwatafutia ajira kitakuwa cha vijana wote wa kitanzania hakitaangalia chama kwa ajili ya kuwatafutia ajira vijana.”alisema Bw Lema.

Kuhusu Sekondari za Jumuiya ya Wazazi CCM

Anasema kilichomsukuma pia kugombea nafasi hiyo ni hali duni ya Shule za Sekondari za Jumuiya hiyo na kwamba mkakati wake sasa ni kufufua shule zote za Jumuiya ili  ziweze kuendana na ushindani wa shule zilizopo ziweze kwenda na kiwango bora cha elimu

Anasema kwa muda mrefu Shule hizo zimekuwa zikitoa elimu duni kutokana na kutokuwepo usimamizi mzuri hivyo ataimarisha miundombinu ya Shule hizo kuhakikisha zinatoa elimu bora kulingana na mahitaji ya kitaaluma ya sasa.

Anasema Shule hizo zinapaswa kuboreshwa ili ziweze kuendana na hali halisi ya sasa na kwamba jukumu hilo la kuziboresha linawezekana kwa kushirikiana na Wazazi wa Jumuiya hiyo ili kufanikisha kuwa na walimu bora pamoja na kutoa taaluma inayokwenda sambamba na mahitaji ya Taifa kwa sasa.

Anasema anachohitaji ni kuungwa mkono na wanachama wa Chama hicho wakati wa uchaguzi utakapowadia ili kwa pamoja waweze kushirikiana kuijenga Jumuiya hiyo muhimu hasa katika wakati huu ambao kumekuwepo na ushindani mkubwa kutoka vyama vya Upinzani.

Hata hivyo jina la Bw Lema sio jina jipya katika medani za siasa hapa nchini kupitia Chama cha Mapinduzi kutokana na nafasi mbalimbali ambazo amekuwa nazo ndani ya Chama hicho ambapo kwa sasa Mlezi jumuiya Wazazi mkoa wa mwanza,

Kuhusu nini kimemsukuma kugombea

Anasema kwa mujibu wa Katiba ya CCM kila mwanachama ana haki ya kugombea kutokana na demokrasia,kuleta mabadiliko na mageuzi ndani ya jumuiya wazazi ili iendane na wakati kiuchumi,iachane kuwa tegemezi ndani ya chama iweze kujitegemea yenyewe

Anataka Jumuiya hiyo iweze kuimarika zaidi na kukisaidia chama na kuboresha maslahi ya watumishi ndani ya jumuiya ili waweze na ari zaidi na nguvu zaidi katika kuitumikia jumuiya na chama hasa wakati huu ambao kumekuwepo na changamoto nyingi kutoka vyama vingine vya siasa.

“Mwaka 2008 nilipoteuliwa kuwa mjumbe wa kukusanya fedha za uchaguzi mkuu wa niligundua mambo mengi ndani ya jumuiya ambayo yako ndani ya uwezo wangu wa kuweza kuyatatua ili Jumuiya iweze kuwa vizuri kiuchumi”.

“Mfano jumuiya ina kiwanja shekilango Dar es Salaam,tunaweza kujenga hoteli ya nyota tano na kuweka na kumbi za mikutano itachangia kuleta mapato ndani ya chama na jumuiya na fedha tunazo kutokana na uzoefu nilionao katika biashara kuweza kukopa fedha benki kujenga hoteli hiyo,fedha zitatumika kujenga chama na kurudisha deni la benki”anasema Bw Lema.

No comments:

Post a Comment

KARIBU