IKIWA imebaki miaka mitatu kabla ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika nchini
mwaka 2015, wabunge wawili vijana wamewataka wakazi wa Mkoa wa Kigoma
kujiandaa kumpata kutoka eneo hilo. Kauli za Wabunge hao
zimekuja kipindi ambacho mchakato wa Katiba unaendelea huku kukiwa na
uwezekano wa umri wakugombea urais kushuka hivyo kuwawezesha wanasiasa
wengi vijana akiwamo Zitto, kugombea nafasi hiyo.
Wakizungumza
katika tamasha kubwa lililokutanisha mamia ya wakazi wa Mkoa wa Kigoma,
Deo Filikunjombe ambaye ni mbunge wa Ludewa (CCM), Joshua Nasari wa
Arumeru Mashariki (Chadema) na Halima Mdee, Kawe (Chadema), walisema
wanaamini Rais wa 2015 atakuwa Mbunge wa Kigoma kaskazini na ambaye ni
mzaliwa wa mkoa huo.Katika kauli yao hiyo, wabunge hao walisema
Mbunge huyo ameonyesha umahiri mkubwa katika kusimamia mambo ya kitaifa
bila upendeleo, jambo linalomfanya kujijengea umaarufu mkubwa ndani na
nje ya nchi, hivyo kuonekana wazi kulibeba vema kundi la Vijana wa Taifa
hili.
Akimzungumzia kuhusu rais ajaye kutoka Kigoma,
Filikunjombe alisema kundi la vijana lazima liungane kuhakikisha kuwa
linatoa viongozi watakaopigania maslahi yao na Taifa kwa jumla ili
kuleta ukombozi wa kifikra na kimaendeleo kwa maslahi ya jamii.
Lazima
mtambue kuwa, Tanzania ni nchi yetu sisi wote na lazima vijana wote
bila kujali itikadi zetu za kisiasa tunatakiwa kujipa moyo kwamba
tunaweza kufanya makubwa katika kuleta maendeleo ya jamii katika nchi
yetu," alisema Filikunjombe na kuongeza:"Vijana wa Kigoma
mnabahati ya kuwa na Wabunge wazuri na ninaamini miaka michache ijayo
lazima mkoa huu utoe Rais wa Tanzania." Huku akishangiliwa na
umati mkubwa wa watu waliokusanyika katika uwanja wa Lake Tanganyika
mjini hapa kuhudhuria tamasha hilo lililopambwa na wasanii nyota wa
kizazi kipya kutoka Mkoa wa Kigoma, Filikunjombe alisema; "Zitto
anastahili kuwa rais".Mbunge huyo wa CCM ambaye katika siku za
karibuni ameonekana kuwa mshirika mkubwa wa kisiasa wa Zitto na Chadema,
alisema Zitto anafaa kuwa Rais kwani amefanikiwa kuwaunganisha watu na
kuleta umoja miongoni mwao, jambo ambalo linadumisha umoja wa kitaifa.
Kauli ya Nassari
Kwa
upande wake Nasari, alisema Mkoa wa Kigoma umejitokeza wazi kuwa na
wanasiasa mahiri na wenye vipaji vya hali ya juu katika kupigania
maslahi ya wananchi pamoja na kupambana na ufisadi unaodidimiza uchumi
wa taifa letu na kuwanufaisha wachache kwa kutumia nafasi zao.‘Leo,
ni mara yangu ya kwanza kufika Kigoma, lakini kwa jinsi ninavyoona
mpangilio mzuri wa shughuli hii, naamini kabisa kuwa, Zitto Kabwe
aliyeandaa hafla hii na kuwakusanya wasanii wa Kigoma kuwa kitu kimoja
anafaa kabisa kuwa rais ajaye wa Taifa letu. Na haya ninayasema kwa
uhakika bila hata chembe ya mzaha," alisema Nasari.
Huku
akishangiliwa na mamia hayo ya wakazi wa Kigoma, alifafanua kwamba
wanasiasa vijana wamejipanga kuwatetea wananchi na hususani kundi la
vijana katika kuondoa matatizo mbalimbali yanayowasibu katika maisha kwa
kuwajengea mazingira mazuri ya kufanya kazi zao za uzalishaji mali.
Mdee amliza Zitto Katika
hatua nyingine, Mbunge wa Kawe Halima Mdee (Chadema) alimliza Zitto
jukwaani baada ya kumuelezea kuwa ni ‘jembe’ katika mambo mbalimbali na
mtu mwenye uchungu na maendeleo ya taifa.Mdee aliyepewa nafasi
ya kuwasalimia Wananchi alisema amekuwa na Zitto tangu Chuo kikuu cha
Dar es Salaam na kwamba kutokana na ujasiri na umahiri wake katuika
kutetea masilahi ya wanyonge na taifa, anafaa kuwa mmoja wa viongozi wa
juu katika Taifa.
Ndugu zangu watu wa Kigoma, kwa kweli mna
bahati sana, achilia mbali kuwa na vipaji katika sanaa ya muziki na
michezo hasa mpira wa miguu, lakini mna wanasiasa wakali ambao ni tishio
hapa nchini. Mimi namkubali sana Zitto Kabwe na ninaamini kuna siku
atakuwa kiongozi wa juu katika nchi yetu," alisema Mdee. Mdee alipongeza ushirikiano wa wananchi wa Kigoma na kusisitiza kuwa unatakiwa kuenziwa na kuigwa na mikoa mingine.
Zitto akiri kutoa machozi
Zitto
alipulizwa na gazeti hili alikiri kudondosha machozi jukwaani kutokana
na Mdee kuzungumza kwa hisia kali na hivyo maneno yake kumchoma na
kushindwa kujizuia jukwaani.
" Kwa weli Halima Mdee aluzumgumza
maneno mazito sana na alinikumbusha mbali enzi za Chuo kikuu tukiwa
kwenye harakati za kutetea maslahi ya wanachuo na pia nimekuwa naye
kwenye harakati za kisiasa ndani ya Chadema, ndiyo maana nilishindwa
kujizuia na kuanza kutoa machozi," alisema Zitto. Alisema
amefarijika kuwaona wabunge wenzake kutoka vyama vya CCM, NCCR Mageuzi,
Chadema na CUF wamefika Kigoma kumuunga mkono katika uzinduzi wa wimbo
wa 'Leka dutigite' ulioimbwa kwa pamoja na wasanii wa muziki wenye asili
ya Kigoma. Zitto alisema Mkoa wa Kigoma kwa muda mrefu umekuwa
nyuma kimaendeleo hivyo, kuufanya kudharauliwa na watu wengi hata kama
hawajui lolote juu ya eneo hilo.
‘Wapo watu wanaotubeza kwamba
mkoa wetu ni masikini na haufai kuishi, na kasumba hii imejengeka hadi
kwa baadhi ya watumishi wa Serikali. Ndiyo maana sishangai ninaposikia
kwamba kuna watumishi wa Serikali wanakataa kuhamia Kigoma. Lakini hii
dhana sasa itaisha," alifafanua Zitto.
Wabunge waliohudhuria
Wabunge
waliofika Kigoma kwenye hafla hiyo ni Mdee , Amina Mwidau wa viti
maalumu (CUF), Esta Bulaya ( Viti maalumu (CCM), Filikunjombe (CCM),
Kangi Lugola wa Mwibara, David Kafulila (Kigoma Kusini, NCCR-Mageuzi),
Nasari (Arumeru Mashariki Chadema) na Raya Ibrahim Khamis wa viti
maalumu kutoka Pemba.Kauli ya Nape
Alipoulizwa Katibu Mwenezi
wa CCM Nape Nnauye kuhusu Filikunjombe kumtabiria Zitto kuwa Rais
wakati anatoka upinzani, alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa
hajasikia wala kulisoma popote.“Nyie andikeni kwanza halafu
ndiyo nitaweza kusema, kwa sasa siwezi kusema chochote kwa sababu
sijasikia kitu chochote ama kusoma popote pale jambo hilo,” alisema
Nape.
No comments:
Post a Comment