Wednesday, 18 July 2012
Rais wa Liberia, Ellen Johnson-Sirleaf awasili nchini Tanzania
RAIS wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf amewasili nchini leo kwa ziara ya siku tatu. Rais huyo kesho atazindua Ofisi ya Mradi wa Viongozi wa Afrika Kudhibiti Malaria (ALMA) jijini Dar es Salaam.
Pia leo mchana atatoa mhadhara katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuhusu umuhimu wa mwanamke katika Maendeleo ya Afrika. Sirleaf aliwasili jana mchana katika Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam wa ‘Terminal one’ kwa kutumia ndege yenye namba N 287DL na kupokewa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete na kupigiwa mizinga 21.
Katika mapokezi ya Rais huyo mwanamke Afrika, Kikwete alifuatana na Mkuu wa Majeshi Davis Mwamnyange, Waziri wa Wanawake Jinsia na Watoto Sophia Simba, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mahadhi Mahadhi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadick.
Rais huyo ambaye ni Mwenyekiti wa ALMA, mara baada ya kuwasili alifanya mazungumzo na Rais Kikwete na baadaye alishiriki katika dhifa ya kitaifa Ikulu jijini Dar es Salaam aliyoandaliwa na Rais Kikwete .
Kesho Rais Sirleaf aliyeko nchini kwa mwaliko wa Rais Kikwete atatembelea kiwanda cha kutengeneza vyandarua cha A to Z kilichopo jijini Arusha na siku hiyo hiyo atarejea nchini kwake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment