SEHEMU YA HOTUBA YA JK
.......Sina
budi kusisitiza kwamba tunapofanya hivyo tunaongozwa na uwezo tulio
nao wa kulipa. Kwa sasa hatuwezi kuwaahidi kuwa tunao uwezo wa
kuwalipa mshahara wa kuanzia wa shilingi 3,500,000/= na posho zote zile. Tukifanya hivyo malipo ya daktari anayeanza kazi yatakuwa shilingi 7,700,000/=. Kwa hakika kiasi hicho hatutakiweza. Si vyema kutoa ahadi hewa kwa watu tunaowaheshimu na kuwathamini kama walivyo madaktari.
Kutokana
na ukweli huo basi kama daktari anayeona kuwa hawezi kufanya kazi
Serikalini bila ya kulipwa mshahara huo awe huru kuacha kazi na kwenda
kwa muajiri anayeweza kumlipa kiasi hicho. Nasi tutamtakia kila la
heri. Hana sababu ya kugoma ili ashinikize kulipwa mshahara huo.
Asisumbuke, hatalipwa mshahara huo. Isitoshe, hana sababu ya kuendelea
kuwa na mgogoro na mwajiri ambaye hana uwezo wa kumlipa anachokitaka.
Huna sababu ya kumpa usumbufu mwajiri wa kukuandikia barua ya
kujieleza au kukuachisha kazi. Kwa nini upate usumbufu wa kupata
barua hizo na kuzijibu. Kwa nini upate usumbufu wa kuachishwa kazi na
kutakiwa kuondoka kwenye nyumba ya Serikali ndani ya saa 24. Jiepushe
na yote hayo kwa kujiondoa mwenyewe. Usipofanya hivyo, mwajiri
anakuwa hana jinsi bali kukuondoa kazini maana unakwenda kinyume na
sheria za kazi na maadili ya kazi ya udaktari.
Mamlaka za ajira zimeanza kuchukua hatua hizo na wataendelea kufanya
hivyo kwa wote wanaoendelea kugoma. Najua baada ya hatua hizo
kuchukuliwa kuna manun’guniko ya kuonewa. Hivyo, mlitegemea mwajiri
afanyeje? Ni bora kufanya hivyo ili ajue hana daktari aweze kufanya
utaratibu wa kuziba hilo pengo na huyo ajae awe na mahali pa kuishi.
Vinginevyo atakuwa anajidanganya kuwa anae daktari ambae hayupo kazini
na wala hataki kufanya kazi.
No comments:
Post a Comment