Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, (NUU) Mhe.
Edward Lowassa( Mb) akiwa na Kaibu Balozi wa Ubalozi wa Kudumu wa
Tanzania katika Umoja wa Mataifa. Mhe.Lowassa akiwa na wabunge wanne
wamekamilisha ziara yao ya kikazi na mafunzo, ziara ambayo ilikuwa na
lengo la kujionea hali ya utendaji kazi katika vituo vya Ubalozi nchi
za nje, kujua mafanikio, matatizo na changamoto wanazokabiliana nazo
watendaji, ikiwa ni pamoja na namna ya kutafuta njia bora zaidi za
kuimarisha utendaji wa kazi ili uwe wenye tija zaidi. Aidha Kamati
hiyo ilipata fursa pia ya kutembelea na kukagua mali zinazomilikiwa na
serikali hususani majengo.
Na Mwandishi Maalum.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ( NUU) Mhe. Edward
Lowassa (Mb), amewaasa Maafisa wa Ubalozi wa Kudumu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, kutotetereka wala kuyumba
pale inapowapasa kutoa misimamo kwa maslahi ya nchi yao.
Ametoa
wasia huo wakati alipokuwa akitoa majumuisho ya ziara ya kamati yake,
ziara ambayo pamoja na mambo mengine ililenga kujifunza na kujionea
hali hali ya mazingira ya utendaji kazi ya maafisa wanaoiwakilisha
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
Akimnukuu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mhe. Lowassa alikuwa na haya ya kusema.
“
Mwalimu aliwahi kutueleza huko nyuma kwamba, jambo linaloipa heshima
kubwa Tanzania licha ya umaskini wake ni namna isivyotetereka katika
kukisema na kukitetea kile inachokiamini hata kama kinawaudhi wakubwa.
Kwa hiyo nami ninapenda kwanza, kuwapongeza kwa utendaji wenu wa
kazi, lakini kubwa na la msingi msiogope kutetea misimamo ya nchi yenu
licha ya umaskini wetu” akasema Mwenyekiti wa Kamati.
Akizungumza
kwa niaba ya wajumbe wa Kamati hiyo inayowajumuisha Mhe.Beatrice
Shelukindo,Mhe. Rachel Masishanga, Mhe. Khalifa Khalifa na Mhe. Vita
Kawawa. Mhe. Edward Lowassa, licha wa kuwaasa maafia hao kutolegeza buti
zao pale linapokuja suala la kusimamia na kutetea maslahi ya taifa na
utaifa. Amewapongeza maafisa hao kwa namna wavyofanya kazi kwa uhodari
mkubwa ikiwa ni pamoja na ushirikiano wa hali ya juu wanaouonyesha
miongoni mwao.
No comments:
Post a Comment