..

..
.

Tuesday, June 12, 2012

WANAJESHI WA MAREKANI WAENDELEA KUJINYONGA

Visa vya wanajeshi wa Marekani wanaojinyonga vimeongezeka mwaka huu na kuzidi wale wanaouawa nchini Afghanistan.

Takwimu zilizotolewa na idara ya ulinzi zinaonyesha kwamba wanajeshi watano hujinyonga kila siku katika kipindi cha miezi mitano mwaka huu.

Haijabainika sababu za wanajeshi hao kujinyonga. Hata hivyo kuna uwezekano kwamba baadhi wanaona vigumu kuendelea kushiriki vita.

Aidha kumeripotiwa visa zaidi vya dhuluma za ngono, ukatili wa nyumbani na ulevi wa kupindukia.

No comments:

Post a Comment

KARIBU