Hii ilikuwa mechi ambayo ilikuwa na ubunifu mdogo sana huku ikichezwa kwa kasi ya chini sana .
Laureant
Blanc aliteua kikosi ambacho kilicheza mfumo ambao kila mmoja
alitarajia mfumo wa 4-3-3, huku Florent Malouda akihangaika mbele
akitokea katikati ya uwanja.
Roy
Hodgson aliwashangaza watu wengi kwa kumpanga Alex Oxlade Chamberlain
ambaye alicheza upande wa kushoto huku James Milner akicheza upande wa
kulia na Danny Welbeck akiongoza mashambulizi .
Kama
ilivyotarajiwa, Ufaransa ilitawala sana mpira kwa maana ya umiliki
huku ikimaliza kwa wastani wa asilimia 65 ya umiliki wa mpira huku
wakipiga mashuti 21 tofauti na England ambao walipiga mashuti matano
pekee. Hata hivyo mashuti mengi ya Ufaransa yalikuwa ya mbali yasiyokuwa
na madhara ukiachilia mbali shuti la Nasri ambalo lilizaa bao la
kusawazisha, yote kwa yote Ufaransa walihangaika kutengeneza nafasi za
wazi.
Vita ya Mfumo
Ilikuwa
vita nyepesi. England walikuwa na makundi ya wachezaji wanne wanne
kwenye ulinzi na kiungo huku Ashley Young na Welbeck wakicheza mbele -
Laureant Blanc alimpa Alou Diarra maelekezo ya kumkaba Ashley Young na
kumnyima nafasi ya kufanya kazi kwa uhuru hasa pale ambapo Young
alikuwa anarudi chini kusaka mpira. Yohan Cabaye alikuwa akicheza juu
karibu na sehemu aliyokuwa Gerard na Malouda alikuwa akijaribu kumvuta
Scott Parker kutoka kwenye nafasi yake aliyokuwa. Kiujumla kulikuwa na
nafasi finyu sana kwa Ufaransa kufanya mambo yake kwa uhuru kwani
England walijaza upande wao na kuwanyima Ufaransa uhuru wa
kupiga pasi walizohitaji kupanga mashambulizi. Ufaransa walijaribu
mbinu ya kupitisha mipira jambo ambalo liliwafanya England kutoa mipira mingi iliyoza kona ambazo hazikuzaa matunda .
No comments:
Post a Comment