..

..
.

Friday, 22 June 2012

Tanzania yajiandaa kufufua mpango wa Jeshi la Kujenga Taifa


Tanzania inajiandaa kurejesha mpango wa taifa wa jeshi la Kujenga Taifa, ambao ulisitishwa miaka 20 iliyopita, kufuatia wito wa kufufuliwa kwa shughuli hizo kama chombo cha mshikamano wa kijamii.
Vikosi vya ulinzi vya jeshi la Tanzania wakicheza gwaride Dar es Salaam. Serikali ilitenga pesa katika bajeti ijayo ili kurejesha mpango wa taifa wa Jeshi la Kujenga Taifa. [Na Mwanzo Milinga/AFP]
Mpango huo ni mafunzo ya kijeshi ya mwaka mmoja ambapo Watanzania watatakiwa kushiriki kabla ya kujiunga na taasisi za elimu ya juu.
Mpango wa jeshi la Kujenga Taifa ulianzishwa mwaka 1963 na rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere. Ulisitishwa mwaka 1994 baada ya ukosefu wa fedha.
Pamoja na mafunzo ya kijeshi yenye kiwango, mpango huu pia hutoa mafunzo juu ya haki za binadamu, elimu ya uraia, na historia ya Tanganyika na zanzibar, na pia unakusudiwa kuamsha hisia za umoja na uzalendo kwa wanafunzi.
Waziri wa Fedha wa Tanzania William Mgimwa aliliambia bunge wiki iliyopita kuwa kisasi cha shilingi bilioni 7.5 (dola milioni 4.7) zitatengwa katika bajeti ijayo ili kufufua mpango wa Jeshi la Kujenga Taifa.Kwa kuanzia, wanafunzi 5,000 tu wahitimu wa elimu ya juu watachaguliwa kushiriki katika mpango huo.
Makala zinazohusiana

No comments:

Post a Comment

KARIBU