..

..
.

Thursday, June 7, 2012

   TANESCO TANGA BWAWA LA MTERA
TANESCO TANGA KUTOA ONYO KUHUSU  WIZI WA KUJIUNGANISHIA              UMEME MAJUMBANI
KITENDO cha watu kujiunganishia umeme kinyemela pamoja na wizi wa miundombinu ya umeme, ni moja kati ya changamoto zinazolikabili shirika la Umeme mkoa wa Tanga hali iliyopelekea kulipa hasara shirika hilo.
Meneja wa Tanesco Mkoa wa Tanga,Samweli Makalla amesema hayo wakati akizungumza na Mwambao fm   ofisini kwake  ambapo amesema kuwa hivi sasa wanaendelea na msako katika maeneo  yote sugu kwa wizi huo kwa kushirikiana na jeshi la polisi.
 Makalla amesema kuwa baadhi ya maeneo sugu ambayo miundo mbinu huibiwa ni Pongwe,Kichangani, na Barabara ya kuelekea Muheza na maeneo yote korofi watahakikisha wanapitisha msako mkali ili kuweza kuwabaini wezi wa miundo minu hiyo na kuwachukulia hatua zinazostaili.
 Pamoja na hayo meneja huyo amesema kuwa  changamoto nyengine inlolikabili shirika hilo  ni juu ya wateja wao  kushindwa kulipa  bili za umeme kwa wakati ambao umekuwa kikwazo cha maendeleo  katika shirika hilo.
 Hata hivyo ametoa wito  kwa watu wanoharibu  miundo mbinu na kujiunganishia umeme katika njia zisizo za halali  kuacha tabia hiyo  mara moja kwani atakaye bainika atachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani
......................................................................................................................................................

No comments:

Post a Comment

KARIBU