MKOA WA RUKWA
Anwani ya Simu: “REGCOM”
SIMU:(025)-2802137, 2802138,2802187
FAX NA. (025) 2802217
OFISI YA MKUU WA MKOA
S.L.P. 128,
SUMBAWANGA.
----
Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa Rukwa inapenda kuutangazia Umma kuwa imepotelewa na
vitabu ishirini (20) vya leseni za biashara vilivyopotea tarehe 22 Mei
2012 katika moja ya Daladala Jijini Dar es Salaam.
Vitabu hivyo vilivyotolewa na Wizara ya Viwanda na Biashara vikiwa na kumbukumbu namba 1389501 mpaka 1391500.
Kwa
yeyote atakayeona vitabu hivyo au kuvinunua anaombwa avipeleke kituo
chochote cha polisi kilicho karibu yake au kutoa taarifa juu ya mwenye
navyo katika kituo hicho.
Ifahamike
kuwa vitabu hivyo ni batili hivyo haviruhusiwi kutumika kwa namna
yeyote ile. Na atakayethibitika kuvitumia atachukuliwa hatua kwa mujibu
wa sheria zilizowekwa.
Ewe mfanyabiashara, epuka manunuzi na matumizi ya vitabu vyenye namba tajwa hapo juu kwa usalama wa biashara yako.
Kwa mawasiliano tunaomba mtumie namba zetu hapo juu.
Tunaomba ushirikiano wenu.
No comments:
Post a Comment