Kaka mkubwa wa marehemu
aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward Ogunde,
George Ongiri Ogunde (wa kwanza kulia) akishirikiana na ndugu, jamaa
na waandishi wa habari, kubeba mwili wa mhariri huyo, aliyefariki
dunia ghafla jana usiku eneo la Forest Hill, mjini Morogoro. Mwili huo
ulikuwa unatolewa chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Rufaa ya
mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam
kwa maandalizi ya mazishi katika Kijiji cha Mugumu kilichopo wilaya
ya Serengeti, mkoani, Mara..
Mbunge wa Jimbo la Morogoro,
Azizi Abood, akiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari
(2006), Husein Bashe wakisubiri kuuona mwili wa Willy Edward
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel
Bendera (kulia) akisikiliza jambo kutoka kwa kaka mkubwa wa marehemu
aliyekuwa mhariri mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward Ogunde,
George Ongiri Ogunde muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kwenda jijini
Dar es Salaam kwa maandalizi ya mazishi katika kijiji cha cha Mgumo
kilichopo wilaya ya Serengeti mkoani Musoma. wa pili kutoka kulia ni
Katibu Tawala wilaya ya Morogoro, Alfred Shao na kaka mkubwa upande wa
baba, Isack Ugunde.
No comments:
Post a Comment