mzee majuto akiwa sharobaro
Nguli
wa sanaa ya vichekesho Bongo, Amri Majuto ‘Mzee Majuto’
amesema anakaribia kuachana na fani hiyo iliyomletea umaarufu na
heshima kubwa kote nchini.
Katika
mahojiano ya dakika 30 aliyofanya na mtandao huu akiwa wilayani
Bagamoyo Mzee Majuto alisema kuwa anataka kufanya kazi zake mwenyewe
sambamba na vijana wachache aliowachagua kuepuka dhuluma
anayokutana nayo kutoka kwa wajanja wanaotajirika kupitia migogo yao
huku wakitoa malipo kiduchu kwa wasanii.
“Binafsi
nalipwa Laki tano mpaka sita kwa filamu moja ambayo nina uhakika
mtengezaji anakwenda kuingiza zaidi ya milioni themanini, sasa
kuna haja gani mimi kuendelea kufanya kazi hizo”, alihoji Mzee
Majuto.
Akiendela
zaidi mchekeshaji huyo mwenye heshima kipee kwa wapenzi wa filamu
nchini alisem akuwa si kama anaacha kuigiza moja kwa moja lakini
atahamia katika kufanya kazi zake binafi tofauti na hizi za watu ili
aweze kunufaika na jasho lake .
No comments:
Post a Comment