Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akiwa na Dkt Asha-Rose Migiro
katika hafla ya kumuaga rasmi iliyofanyika leo katika Makao Makuu ya
Umoja wa Mataifa baada ya kumaliza muda wake kama Naibu Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa
Mashirika
ya Umoja wa Mataifa yanayohusika na masuala ya Idadi ya Watu
(
UNFPA),Ugonjwa wa Ukimwi ( UNAIDS) na Mpango wa kupambana na Ugonjwa
wa Malaria ( RBM) jana jumanne yaliandaa tafrija kamambe ya kumshukuru
na kumuaga Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha-Rose
Migiro.
Tafrija
hiyo ya aina yake na ambayo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akiambatana na mke wake na kuhudhuriwa
pia na wadau mbalimbali akiwamo Mtendaji Mkuu wa UNDP Bi Helen
Clark, mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika UM, sekta binafsi na
taasisi za kiraia imefanyika hapa makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Akizungumza
wakati wa tafrija hiyo, Katibu Mkuu Ban ki Moom ameleezea baadhi ya
sababu zilizomsukuma kumteua Dkt. Asha- Rose Migiro kuwa msaidizi
wake wa karibu.
“
Nilianza kumfahamu Asha- Rose Migiro wakati huo sote tukiwa mawaziri
wa mambo ya nje katika nchi zote. Uwezo wake na uelewa wake wa mambo
ulinivutia sana, lakini nilivutiwa zaidi pale nilipofahamu kwamba
aliwahi kuwa waziri anayehusika na masuala ya wanawake na watoto.
Nikajiridhisha kwamba huyu ndiye alikuwa ananifaa kuwa msaidizi wangu wa
karibu” akasema Ban Ki Moon na kuufanya umati ulihohudhiria tafrija
hiyo kushangilia kwa nguvu.
Kama
hiyo haitoshi, Ban Ki Moon amemuelezea Dkt. Asha- Rose Migiro kama
msaidizi wake wa karibu ambaye licha ya kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa
lakini ni mtu ambaye alikuwa hana makuu na wala hata siku moja
hakujikweza.
“
Katika kipindi chote ambacho Migiro amekuwa msaidi wangu wa karibu,
amenisaidia katika mambo mengi, ni mtu muadilifu sana, ni mtu
aliyekaribu sana na watu, aliyeamsha matumaini na kuwapa tabasamu watu
waliokuwa katika mazingira magumu. Daima amekuwa mstari wa mbele
kunisaidia na hakuna hata siku moja alipojikwenza. Na kwa sababu hii
anastahili tafrija hii” akasisitiza Ban Ki Moon.
Aidha
Ban Ki Moon akamuelezea Asha- Rose Migiro kama kiongozi ambaye daima
alitoa kipaumbele cha aina yake katika masuala ya afya ya jamii eneo
alilotumia uwezo wake wote, maarifa yake yote kama naibu katibu mkuu
kupigania afya ya wanawake na watoto na watu wote walio katika mazingira
magumu
No comments:
Post a Comment