Mcheza
sinema maarufu duniani kutoka nchini Marekani Deidre Lorenz atakimbia
mbio za kila mwaka za Mount Kilimanjaro Marathon zinazoanza kutimua
vumbi kuanzia tarehe 24 Juni mwaka huu kutoka Moshi Club mjini Moshi.
Mbio
hizi zilizoanzishwa na mama Marie France kutoka katika mji wa
Bethesda, Maryland nchini Marekani mwaka 1991 ni mbio zinazojulikana
kama 7 continental Races na zimeshawahi kupata tuzo mbalimbali za
kimataifa.
Ujio
wa mcheza sinema huyu aliyecheza sinema nyingi kama vile Santorini
Blue, Perfect Strangers, The Great Fight, na nyingine nyingi
unaiweka Tanzania katika macho ya dunia na kuwavutia watalii wengi
kutoka taifa hili tajiri duniani. Deidre Lorenz alizaliwa katika jiji la
Oregon nchini Marekani lakini akahamia katika jiji la New York City
linalijulikana kama "The Big Apple" nchini Marekani akiwa na kampuni
yake ya kutengeneza sinema inayoitwa Thira Films LLS.
eidre
Lorenz ameshawahi kuteuliwa zaidi ya mara tatu kugombe tuzo za wacheza
sinema maarufu duniani zinazojulikana kama Grammy Awards. Mcheza sinema
huyu ataambatana na Wamarekani wengine kuja nchini tarehe 21 Juni
kukimbia mbio hizi ambazo zimetokea kuutangaza sana mji wa Moshi tangu
mwaka 1991. Lorenz alipatikana katika bahati nasibu iliyochezwa wakati
wa mbio za New York Marathon mwaka jana.
Naye
mwanzilishi wa mbio hizi mama Marie Frances ana historia ya kuanzisha
mbio na matamasha mbalimbali duniani. Alikuwa pia mwanzilishi wa mbio za
Pyramid Marathon nchini Misri pamoja na Miss Universe Egypt matamasha
yaliyojizolea sifa kemkem.Aliombwa kuja kuanzisha mbio za Marathon
nchini Tanzania na balozi wa Tanzania wa wakati ule nchini Misri.Mbio za
Mt. Kilimahjaro Marathon ni moja kati ya mbio tafauti za marathon
zinazifanyika katika mji wa Moshi.
Mount Kilimanjaro Marathon
zitaanzia Moshi Club mpaka Rau madukani na kurudi mara tatu ambazo
zitakuwa kilimeta 42. Kutakuwa pia na mbio z akilometa 21, kilimeta 10
na kilometa 5 kwa watoto. Wakimbiaji hawahitaji kuwa na ujuzi wa
kukimbia watu wote wanaweza kukimbia.
No comments:
Post a Comment