Katika kuifanya ligi kuu ya Spain
iwe ya ushindani serikali ya nchi hiyo imesema imeanza kuchukua hatua
kadhaa moja wapo kuongea na giants wa soka nchini Hispania Real Madrid
na Barcelona ambao wanaweza wakawa tayari kushea faida ya haki za
matangazo ya Televison miongoni mwa vilabu vya La Liga, kwa mujibu wa
Waziri wa Michezo wa nchi hiyo.
Jose Ignacio Wert alisema: "Naamini kwamba Madrid na Barcelona wapo
tayari kuweza kushea mapato yatokanayo na kuuza haki za matangazo ya TV.
Vilabu kwenye La Liga huwa vina utaratibu wa kuongea kila mmoja
kimpango wake na wamiliki wa TV, tofauti na ligi nyingine barani ulaya
ambazo zina mfumo wa kuungana kwenye suala la haki za matangazo ya TV.
Real na Barca wanapata nusu ya mapato yote yatokanayo na kuuza haki za
matangazo ya mechi - nusu ya £511million.
Utafiti uliotoka mwezi April na chuo kikuu cha Barcelona, ulionyesha
kwamba kwenye msimu wa 2010-11 Barca walipata kiasi cha £130 kutokana
na haki za matangazo ya TV, Madrid walipata £124million huku Valencia
wakipata £33.5million.
No comments:
Post a Comment