Golikipa wa timu ya taifa ya Spain Iker Casillas amefikia rekodi mbili kubwa katika mechi za kirafiki hivi karibuni.
Katika mechi ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Serbia wikiendi iliyopita
ilikuwa mechi ya 73 kwa golikipa wa Real Madrid kutoruhusu wavu wake
kuguswa katika mechi 130 za kimataifa - na kumfanya kuipita rekodi ya
zamani iliyokuwa imewekwa na golikipa wa zamani wa Uholanzi Edwin van
der Sar.
Ushindi wa siku ya jumatano ya juzi dhidi South Korea, kwenye mechi
ambayo Casillas aliingia kama mbadala wa Pepe Reina, ulikuwa ushindi wa
95 kwa Caillas kwenye 130 alizoichezea Spain. Hilo lilimfanya awapite
mlinzi wa zamani wa Ufaransa Lilian Thuram na babu wa Misri Ahmed
Hassan.
Ahmed Hassan anashikilia rekodi ya kucheza mechi nyingi za kimataifa,
akiichezea Misri mechi 181. Ikiwa Casillas atakuwa safi kiafya na uwezo
wake ukiendelea kuwa juu basii inatabiriwa kuwa mpaka 2017 ambapo
atakuwa na miaka 36 atakuwa amemfikia Ahmed.
No comments:
Post a Comment