..

..
.

Monday, 28 May 2012

   EEE HII NDIO IMAN THABIT SIYO LELEMAMA KAMA WAISLAM WA BARA



                                                         KANISA la Assemblies of God liliopo 
Kariakoo mjini Unguja, limechomwa moto na kuharibiwa vibaya katika vurugu zilizoibuka jana asubuhi.

Waumini wa kanisa hilo walishindwa kufanya Ibada ya Jumapili katika kanisa hilo kutokana na uharibifu mkubwa huku wakiwa na hofu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Aziz Juma alithibitisha kuchomwa moto kwa kanisa hilo juzi usiku wa saa nne na gari moja aina ya Corolla kuharibiwa vibaya.

“Ni kweli Kanisa la Assemblies of God liliopo Kariakoo limechomwa moto na watu wasiojulikana na uchunguzi zaidi kujuwa nani waliohusika unaendelea,” alisema Juma.

Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo, Dickson Kaganga alisema watu wasiojulikana, walivamia
kanisa hilo saa nne za usiku juzi na kuanza kuwashambulia walinzi ambao walizidiwa na kukimbia.

Kaganga alisema uharibifu mkubwa umefanyika ndani ya kanisa hilo na vifaa vya muziki na vipaza sauti vyote vimeharibiwa.

“Kanisa limeharibiwa vibaya na linahitaji matengenezo makubwa sehemu ya ndani na nje,” alisema. Kanisa hilo lilivamiwa na kutiwa moto mara baada ya viongozi wa Jumuiya ya Kiislamu ya Uamsho kukamatwa na Polisi kwa kufanya maandamano kinyume cha sheria.

Askofu Kaganga aliitaka Serikali kufanya uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo ambalo linahatarisha amani na utulivu pamoja na uhuru wa kuabudu.

1 comment:

KARIBU