Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza ndg CLEMENT MABINA ameuwawa
na wananchi wenye hasira kali kwa kupigwa mawe huko maeneo ya Kiseke
jijini Mwanza
Chanzo cha kuuwawa ni kwamba mabina aliwanyang'anya ardhi wananchi hao
na kesi ikawa mahakamani na leo mchana Mabina bila kibali cha mahakama
alikuwa anapanda miti na kujenga msingi wa nyumba ndipo wanachi wakaenda
kumhoji iweje anapanda miti na kuweka msingi kwenye viwanja hivyo
ilhali kesi ipo mahakamani?
Mabina akaanza kutoa lugha chafu na kurusha risasi hewan
Risasi zilipomuishia na kufanikiwa kumuua raia m1 kwa risasi ndipo
wananchi wenye hasira kali wakamrudia kumpiga wakiwa na mapanga, mawe na
kila dhana ya kijadi, jambo lililopelekea umauti kumkuta. Mauaji
yametokea mchana huu majira ya saa 7.
No comments:
Post a Comment