Hapo tarehe 3 Julai, kampuni ya Tullow Oil plc, kampuni ya utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi iliyoko London, ilitangaza kuwepo kwa akiba za ziada za mafuta katika bonde la Ziwa Turkana ambako ilianza uchimbaji mwezi Mei. Tarehe 19 Julai, Kampuni ya Cortec Mining Ltd ilitoa matokeo ya kuthibitisha ugunduzi mpya wa madini adimu yenye thamani ya hadi kufikia dola bilioni 62.4 na hifadhi za niobium zinazokadiriwa kuwa na thamani ya dola bilioni 35 katika Kusini Mashariki ya Kenya.
"Hiki mpaka sasa ni kiwango kikubwa zaidi cha akiba ya madini nchini Kenya," Mkurugenzi Mwendeshaji wa kampuni David Anderson alisema wiki iliyopita mjini Nairobi. "Ugunduzi huo katika Kilima Mrima [huko Kwale] kutaiweka Kenya katika nafasi ya kuwa na nguvu miongoni mwa nchi wazalishaji wakubwa wa madini adimu duniani."
Ugunduzi wa hivi karibuni umezidisha miito ya wadau na waangalizi wa sekta hii kwa serikali kufuatilia kwa haraka Muswada wa Uchimbaji wa madini na Madini ya mwaka 2013, na kusitisha utoaji wa vibali vipya wakati huu wa mpito.
Mpaka hapo muswada utakapopitishwa, serikali kwa kutumia Sheria ya Uchimbaji ya mwaka 1940 kutoa vibali vipya, ambavyo kwa mujibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Madini ya Kenya, imepitwa na wakati na sheria isiyofaa kwa kushughulikia changamaoto za kisasa za uchimbaji na makubaliano ya mikataba.
Kwa mfano, moja ya matatizo ni kwamba baadhi ya makampuni ya kigeni yanapata vibali vya kuchimba kutoka serikalini kwamba yanaweza kuendelea hadi yatakapoweza kuuza madini yao kwa watu wa tatu kwa faidi, Afisa Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Wachimbaji ya Kenya Monica Gichuhi aliiambia Sabahi.
Ili kuzuia tabia hizi na niengine chafu zinazokwamisha maslahi ya Kenya, serikali inapaswa kusimamisha utoaji wa vibali vipya hadi pale muswada mpana utakapopitishwa, alisema.
Muswada huo kwa sasa uko katika ofisi ya mwanasheria mkuu wa Kenya, ikisubiri nyongeza kutoka kwa serikali za majimbo, jamii, vikundi vya kushinikiza, wachimbaji madini, umma na vyombo vingine vyenye maslahi yake huko.
Ulinzi unahitajika ndani ya Muswada mpya
Sheria mpya inapaswa iwe pana na inayotafakari wazo zuri la sera ambayo inashughulikia vipindi vya ukodishaji wa machimbo, mgawano wa mirahaba, ulinzi na usimamizi wa mazingira, na vipi jumuiya za wenyeji zinaweza kufaidikia kutoka na kujihusisha na madini na miradi ya uchimbaji, alisema mwenyekiti wa Jumuiya ya Jiolojia ya Kenya Gladys Karegi Kianji."Ninaelewa Wakenya wamehamasika sana na ugunduzi wa madini haya mapya na mafuta lakini ninashauri kwamba tuwe waangalifu sana ili tusijinasa katika biashara ya faida ya upande mmoja na kutiliana mikataba na wafanyabiashara wa kimataifa," alisema.
Wilson Ngecu, profesa mshiriki katika Chuo Kikuu cha Nairobi, alisema kwamba uchimabaji wa madini adimu kunaweza kuleta hatari nyingi za kimazingira pia. Serikali inapaswa kuchukua muda wa kuandika rasimu na kutoa sheria inayohusiana nayo isiyopendelea upande wowote, alisema.
"Taka zenye mionzi na tindikali za sumu hutolewa wakati wa uchimbaji kwa sababu madini adimu yana sifa hizo hizo za kemikali, hivyo hujaribu kuziweka pamoja na vitu vingine vyenye mionzi kama vile thorium na uranium," alisema. "Serikali inapaswa kulinda, kupitia misingi ya kisheria, dhidi ya shinikizo kutoka kwa 'watoto matajiri wadhalimu' wanaomiliki makampuni ya kimataifa ya utafutaji wa madini."
Sheria mpya inapaswa kujumuisha vipengele vinavyoyataka makampuni ya uchimabaji kutoa ripoti zinazoelezea kwa urefu mipango yao ya kuzuia hatari za kimazingira, kiuchumi, kijamii, kiafya na kiusalama, Ngecu alisema.
Kwa maoni yake, serikali inapaswa pia kuwekeza na kurahisisha miradi ambayo inatoa miundombinu na nguvu watu zinazohitajika katika sekta ya viwanda, kama vile ujenzi wa barabara, mitandao ya usafirishaji wa reli na kuwapatia wafanyakazi wa migodini mafunzo maalumu.
Kwa sababu uchimbaji maliasili za madini umeziyumbisha nchi nyingi za Afrika, vipi wanasiasa wa Kenya wanashughulikia suala hili litakuwa ni ushahidi kwa uongozi wao na wajibu wa kuiweka mbele nchi kwanza, alisema.
Kwa mujibu wa Brian Mutie, anayefanyakazi katika shirika la maendeleo endelevu la Olive Leaf Foundation la Kenya, na ametafiti juu ya mapengo yaliyopo katika kanuni za uchimbaji nchini Kenya, serikali inapaswa kushughulikia mikataba ya uchimbaji kwa maslahi ya jamii za wenyeji, kwa sababu zinaathiriwa na operesheni nzito za uchimbaji na hazipaswi kuachwa kwa huruma za wamiliki wa migodi.
Njia moja ya kufanya hivi ni kuzijulisha ipasavyo jamii za ndani kuhusu kampuni gani zimepata vibali kwa ajili ya kuendeleza maeneo yao.
"Watu wanapaswa kuwa na habari zote za uchimbaji zinazotumwa kwenye tovuti ya Wizara ya Uchimbaji," alisema Mutite, na kuongeza kwamba yeye anapendelea kuanzishwa kwa Mahakama ya Kusuluhisha Migogoro ya Uchimbaji kwa kuamua kesi za mzozo wowote.
Alisema kuwa mabadiliko yaliyofanywa katika kanuni ya Ushiriki Sawa wa Wenyeji ya mwaka 2012, ambayo inaelezea kuwa kampuni zote za kimataifa za uchimbaji zina umiliki fulani wa eneo husika, hili litawavutia wawekezaji zaidi.
Sheria ya sasa inataka umiliki wa asilimia 35 ya wenyeji, lakini serikali ya Rais Uhuru Kenyetta ilipunguza kipengele hicho kwa asilimia 10 katika muswada mpya.
"Ninakaribisha punguzo kwa sababu Kenya haikuwa na ushindani ikilinganishwa na nchi nyingine za kiafrika zenye madini," Mutie alisema.
Baada ya awamu ya kuwasiliana na umma ambayo imeshamalizika, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu itatoa nakala ya mwisho ya muswada kupelekwa bungeni kwa ajili ya kupitishwa, hata hivyo, bado haiko wazi lini hilo litatokea
No comments:
Post a Comment