Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed
Shein, (wa tatu kulia) akijumuika na Vingozi na Waislamu wengine katika
kuwaswalia Merehemu Sgt. Shaibu Shehe Othman, na Cpl Mohammed Juma Ally katika Msikiti wa Nuru Muhammad, Mombasa mjini Unguja leo. (Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu)
Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wakibeba Jeneza la mwili wa Marehemu Sgt Shaibu Shehe Othman, baada ya kuwasili mjini Zanzibar akiwa ni miongoni mwa wanajeshi 7 waliouwawa kwa kupigwa risasi Jimbo la Darfur nchini Sudan hivi karibuni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, akitia udongo katika kaburi la Marehemu Sgt. Shaibu Shehe Othman, aliyezikwa leo katika makaburi ya Mwanakwerekwe mjini Unguja.
Baadhi
ya Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na Ndugu na Jamaa wa
marehemu Sgt Shaibu Shehe Othman, na Cpl Mohammed Juma Ally wakishiriki
mazishi hayo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, (katikati) na Viongozi na Waislamu, wakiangalia Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania, walipokuwa wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu Sgt. Shaibu Shehe Othman, wakati wa mazishi yake katika makaburi ya Mwanakwerekwe leo.
No comments:
Post a Comment