..

..
.

Saturday, January 5, 2013

Viongozi wa Sudan na Sudan kusini wakutana Addis

(L-R) Pagan Amum, south Sudan chief negotiator, South Sudan's President Salva Kiir, former president of Nigeria Abdulsalam Abubakar, Chief African Union mediator Thabo Mbeki, former Burundi president Pierre Buyoya and President of Sudan Omar Hassan al-Bashir meet during talks in Ethiopia's capital Addis Ababa September 24, 2012. Leaders from Sudan and South Sudan will meet on Sunday for the first time in a year to try to agree on border security so that South Sudan can start exporting oil again, a lifeline for both economies. REUTERS/Tiksa Negeri (ETHIOPIA - Tags: BUSINESS COMMODITIES POLITICS)
Viongozi wa Sudan na Sudan kusini wamekutana Ijumaa(04.01.2013)kuondoa hali ya wasi wasi ambayo imetanda tangu kusini kujitenga mwaka 2011 na kuanza usafirishaji mafuta ili kukwamua uchumi wa nchi hizo unaodidimia.
Hakuna taarifa zaidi zilizojitokeza wakati rais wa Sudan Omar al-Bashir na Salva Kiir wa Sudan ya kusini walipokutana pamoja na waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn, ambaye anajaribu kufanya upatanishi kati ya nchi hizo jirani ambazo zilikaribia kupigana vita mwezi wa Aprili.
Sudan's President Omar Hassan al-Bashir (L) meets his host, the new Ethiopian Prime Minister Hailemariam Desalegn, at the Palace in capital Addis Ababa September 23, 2012. Leaders from Sudan and South Sudan will meet on Sunday for the first time in a year to try to agree on border security so that South Sudan can start exporting oil again, a lifeline for both economies. REUTERS/Tiksa Negeri (ETHIOPIA - Tags: POLITICS BUSINESS CIVIL UNREST)
                   Rais Omar al-Bashir akikutana na waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn
Viongozi wote hao wawili watakutana kwa mara ya kwanza peke yao katika mkutano utakaofanyika hii leo Jumamosi (05.01.2013), limeeleza shirika la habari la Sudan SUNA.
Makubaliano hayakutekelezwa
Sudan na Sudan kusini tayari zimekubaliana mwezi Septemba kuanza tena kwa mauzo ya mafuta na kuhakikisha usalama wa mpaka wao ambao mara kwa mara huzuka mapigano , lakini zilishindwa kufuatilia utekelezaji kutokana na kuwapo hali ya kutoaminiana, hali inayokutikana katika mataifa hayo ya Afrika ambayo yamepigana vita virefu vya wenyewe kwa wenyewe.
BRUSSELS, March 20, 2012 President of South Sudan Salva Kiir Mayardit speaks during a press briefing after meeting with President of European Commission Jose Manuel Barroso (not seen) at the EU headquarters in Brussels, capital of Belgium, March 20, 2012
                                        Rais wa Sudan kusini Salva Kiir Mayardit
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema mvutano huo umesaidia kuongeza umaarufu ndani ya nchi hizo kwa serikali zote kwa kuondoa mtazamo kutoka katika matatizo yao ya kiuchumi na kutapakaa kwa rushwa.
Lakini uchumi wa nchi hizo mbili jirani unategemea sana mapato yatokanayo na nishati na zinahitaji mafuta kusafirishwa kutoka katika visima katika Sudan ya kusini.
Serikali ya kusini mjini Juba ilifunga visima vyake vyote vinavyotoa kiasi ya mapipa 350,000 mwaka mmoja uliopita baada ya kushindwa kukubaliana juu ya kodi ya mauzo ya nje.
Upande wa kaskazini unaitoza Sudan kusini mamilioni ya dola kwa mwezi kwa kupitisha mafuta ghafi katika ardhi yake na kuyauza nje kupitia kituo kilichoko katika bahari ya Sham.
Chini ya makubaliano yaliyofikiwa mwezi Septemba , wamekubaliana kuyaondoa majeshi yao kutoka katika mpaka ambao una umbali wa kilometa 2,000, eneo ambalo kwa kiasi kikubwa linagombaniwa na nchi hizo.Pande zote mbili zinasema eneo kama hilo lisilokuwa na shughuli za kijeshi ni muhimu kabla ya mafuta kutoka Sudan kusini ambayo haina bandari yataweza kutiririka tena kupitia ardhi ya Sudan.

No comments:

Post a Comment

KARIBU