Serikali ya Uganda imeufunga mpaka wake na Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Kongo, ambao umekuwa ukiwanufaisha sana waasi wa M23 kwa kuyatoza kodi
magari yanayoingia Kongo kutoka Uganda na nchi nyingine za Afrika
mashariki.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
Rais Yoweri Museveni aliamrisha kufungwa kwa mpaka wa Bunagana
Jumanne ya wiki hii kufuatia ombi la rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Kongo Joseph Kabila. Kufungwa huku kulithibitishwa na msemaji wa jeshi
la Uganda kanali Felix Kulayigye ambaye anasema ilibidi waufunge mpaka
huo. Eneo la mpakani la Bunagana ndilo lililokuwa la kwanza kutekwa na
waasi wa M23 mwezi wa tano mwaka huu. Hii ni kwa sababu kama eneo la
kibiashara lililoko mpakani lina manufaa mengi sana ya kifedha na
walihitaji pesa hizo kuendeleza vitendo vyao vya uasi.
Ikikumbukwa kuwa mwezi uliopita shirika la habari la Reuters
lilichapisha ripoti ya umoja wa mataifa iliyosema Uganda na Rwanda
zinawafathili waasi wa M23, Kinshasa ilitaka mpaka wa Bunagana kufungwa
ili watu wanaowafadhili M23 wasipate njia ya kuendelea kuwapa msaada.
Ingawa Kanali Kulayigye anasema rais Kabila hakutoa msimamo wake, mwezi
uliopita, akizungumza mjini Kinshasa na waandishi habari kutoka Uganda,
rais Kabila alisisitiza kuwa
Jeshi la Uganda lashika doria
Vifaru vya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo vikiweka kambi katika mji wa mashariki wa Rumagambo.
Jeshi la Uganda limeshika doria pale mpakani ili kuhakikisha kuwa
hakuna magari au watu wanaouvuka mpaka wa Bunagana. Tangu mapigano
makali kuzuka mwezi wa tano kati ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo na waasi wa M23, wakongomani wanaoishi karibu na mpaka wa Bunagana
wamekuwa wakilala nchini Uganda na asubuhi kurudi kwao kwenda kulima na
kuteka maji.
Ahebwa Gideon, naibu kamishna wa wilaya ya Kisoro, wilaya iliyo pale
mpakani anasema wakuu wa wilaya hiyo watajadiliana na washika dau mbali
mbali nchini Uganda kuona wakongomani walio mpakani Bunagana watasaidiwa
vipi. Wafanyibiashara wanaosafirisha bidhaa kama sukari, mafuta ya
kupikia, matunda na vyakula vibichi wamekwama pale mpakani pia. Hawajui
la kufanya ila kuhesabu gharama wanayoipata.
No comments:
Post a Comment