Serikali ya Tanzania inapanga kuhakiki wafanyakazi wa kigeni
walioajiriwa katika sekta binafsi, Waziri wa Kazi na Ajira Gaudensia
Kabaka alitangaza mjini Dar es Salaam siku ya Ijumaa (tarehe 16
Novemba).
Kwa sasa serikali haina data kwa kina zinazowahusu wageni
wanaofanyakazi nchini, na kuifanya hali hiyo kuwa changamoto katika
kutekeleza sera zilizobuniwa kwa ajili ya kuongeza ajira kwa Watanzania,
Kabaka alisema, kwa mujibu wa gazeti la The Guardian la Tanzania.
Vibali vya mtu mmoja mmoja vinatolewa kwa wageni, lakini serikali
haiweki kumbukumbu moja kuu kwa vibali kama hivyo.
Akizungumza katika mkutano wa mwaka wa Jumuiya ya Waajiri Tanzania,
Kabaka aliwahimiza waajiri wawe tayari kutoa taarifa za waajiriwa wao
ili zoezi hilo lifanyike katika sekta zote. Kuanzia mwezi ujao, serikali
itasambaza fomu za uchunguzi kila mwezi kwa waajiri ili kuelezea
jinsia, mishahara na aina ya kazi za waajiriwa wao.
Ukosefu wa ajira kwa vijana hasa unahitaji kushughulikiwa na
serikali, Kabaka alisema, pamoja na mishahara duni ambayo haikidhi
mahitaji kwa viwango vya maisha vinavyotosheleza. Sekta binafsi inaajiri
karibu ya asilimia 97 ya nguvu kazi ya nchi, alisema.
No comments:
Post a Comment