Serikali ya Tanzania ilithibitisha Jumamosi (tarehe 17 Novemba) kwamba pembe za ndovu zenye thamani ya dola milioni1.37 zilizokamatwa na maafisa wa forodha huko Hong Kong hapo Ijumaa zilitokea nchini, gazeti la The Citizen la Tanzania liliripoti.
"Haiwezekani kwa mzigo mkubwa kama huo wa pembe za ndovu kupita
katika bandari bila ya kuhusisha maafisa wa forodha na viongozi
wengine," alisema. "Nimefanya mashauriano ya awali na inspekta mkuu wa
polisi ili kuona jinsi tunavyoweza kulishughulikia jambo hili."
Aliahidi kupambana na ujangili haramu na kumshtaki yeyote anayehusika katika biashara hiyo.
Ukamataji wa wiki uliyopita ulitokea chini ya mwezi mmoja baada ya viongozi wa forodha wa Hong Kong kugundua karibia tani nne za pembe za ndovu za magendo zilizosafirishwa kutoka Kenya na Tanzania.
No comments:
Post a Comment