..

..
.

Thursday, October 18, 2012

UJIO MPYA WA KIPINDI CHA "BONGO DAR ES SALAAM"
Ile show iliyokuwa maarufu kwenye kituo cha runinga cha TBC1, ‘Bongo Dar es Salaam’ inatarajia kurejea kwa kishindo kwenye screen.

Staa wa show hiyo Kulwa Kikumba maarufu kama Dude amezungumza kuhusu kuanza tena kwa show hiyo ambayo ipo kwenye hatua ya kurekodiwa.


“Tunarekodi michezo mingi zaidi ili tukianza kuirusha hatupumziki,” anasema Dude.

Amesema ili kuufanya ujio wa show hiyo kuwa wa kishindo zaidi ameamua kuwashirikisha mastaa wa muziki nchini wakiwemo Bahati Bukuku ,Madee,Tunda ,Baby Madaha na Chid Benz.

Dude alisema makubaliano yakifikiwa watashuti wiki hii huku kambi ikiwa Lamada Hotel.

Baby Madaha ameithibitishia Mpekuzi kuhusu kushiriki kwenye mchezo huyo.

No comments:

Post a Comment

KARIBU