..

..
.

Friday, 7 September 2012

WAISLAMU WAVAMIA MAKAO MAKUU YA POLISI JIJINI DAR LEO

Baadhi ya Waislamu wakiwa nje ya jengo la Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani leo.
Polisi wakiimarisha ulinzi wakati wa maandamano hayo.
Moja ya bango walilokuwa nalo waandamanaji hao.
Waandamanaji waliamua kuswali eneo hilo la wizara wakati polisi wakiimarisha ulinzi.
Kamanda Kova akiwa eneo la tukio baada ya kumaliza mazungumzo na viongozi wa waandamanaji.
Rais wa Tamsia Taifa, Sheikh Jaffar Said Mneke (katikati), akiongea na waandamanaji mara baada ya kumaliza kikao na viongozi wa wizara.
Barua inayoonyesha madai wa waandamanaji hao.
Baadhi ya Waislamu jijini Dar es Salaam leo wameandamana kuelekea Wizara ya Mambo ya Ndani kutaka wenzao waliokamatwa wakati wa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linaloendelea nchini kuachiwa. Katika maandamano hayo viongozi wa Waislamu na maofisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani walikutana na kufikia makubaliano kuwa wote waliokamatwa wakipinga zoezi la Sensa Zanzibar na Tanzania Bara wataachia huru. Pia waandamanaji hao wamekubaliana kufanya maandamano mengine ya kumng'oa Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Shaban Bin Simba kwa kutoonesha ushirikiano nao.

No comments:

Post a Comment

KARIBU