..

..
.

Tuesday 28 August 2012

Mohammed alitoa wito wa kufanya vurugu dhidi ya Wakenya



                                        SHEIK  ABOUD ROGO MOHAMMED
Mohammed alikuwa amewekwa kwenye orodha ya vikwazo ya Marekani mwezi Julai "kwa kujihusisha na vitendo ambavyo ama moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja vinahatarisha amani, usalama au utulivu wa Somalia," hasa hasa kwa kuwapa mafunzo na kukusanya fedha kwa ajili ya al-Shabaab.
Mohammed" aliwataka watu wanaomsikiliza kwenye mihadhara yake kusafiri kwenda Somalia kujiunga na al-Shabaab kupigana dhidi ya serikali ya Somalia," ilisema idara ya Hazina ya Marekani.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliweka vikwazo vya kusafiri na kuzuia mali za Mohammed hapo Julai, likisema alikuwa ametoa "msaada wa kifedha, vitu, mafao au ufundi kwa al-Shabaab."
Alikuwa "kiongozi mkuu wa kiitikadi" wa kundi la Hijra la Kenya, ambalo pia linajulikana kama Kituo cha Vijana wa Kiislamu," ulisema Umoja wa Mataifa. Kundi hilo linachukuliwa kuwa mshirika wa karibu wa al-Shabaab kwa Kenya.
Mohammed "alilitumia kundi hilo lenye msimamo mkali kama njia ya kupandikiza siasa kali na kuwapa mafunzo Waafrika wanaozungumza Kiswahili ili kushiriki mambo ya uasi nchini Somalia," kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Kituo cha Vijana wa Kiislamu chatishia kulipiza kisasi

Katika ukusara wake wa Twitter, Kituo hicho cha Vijana wa Kiislamu kilitoa onyo kali kwamba "makafiri (watu wasioamini Mungu) watalipa" kwa kifo cha Mohammed. Wakiweka picha ya bomu la kwenye gari likilipuka barabarani, Kituo hicho kimesema, "Mwanzo tu wa kile kijacho au sio?"
"Kituo cha Vijana wa Kiislamu kimepeleka ujumbe kwa mujahidina wa Tanzania kuhusu ripoti za kifo cha Sheikh Rogo," lilisema kundi hilo, likionesha kwamba linaweza kutanua kisasi chake hadi nje ya Kenya.
Kiongozi wa kituo hicho, Sheikh Ahmad Iman Ali, alisema katika ujumbe uliotumwa kwenye Twitter, "Tupo kwenye njia sahihi pale viongozi wetu wanapopata shahada (wanapokufa mashahidi)."
"Atabakia nyoyoni mwetu daima," kiliongeza Kituo cha Vijana wa Kiislamu.
Polisi nchini Kenya walimkamata Mohammed mwezi Januari, wakishikilia silaha, milipuko na vifaa vya kutegea mabomu. Alipelekwa mbele ya mahakama ya Mombasa tarehe 14 Agosti kwa mashitaka ya kupanga mashambulizi katika maeneo ya umma.
Mohammed alishitakiwa kwa mashitaka sita yanayohusiana na kumiliki silaha isivyo kihalali, ambayo aliyakana na baadaye akaachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni 5 (dola 60,000). Kesi hiyo iliahirishwa na ilikuwa imepangwa kusikilizwa tena tarehe 15 Oktoba.

Kiongozi mkuu wa mafunzo wa Kituo cha Vijana wa Kiislamu awekewa vikwazo

Wakati huo huo, Kamati ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa imemuwekea vikwazo vya kusafiri na kuzuiwa kwa mali zake dhidi ya Abubakar Sharif Ahmed, mmoja wa viongozi wa Kituo cha Vijana wa Kiislamu na "mshirika wa karibu" wa Mohammed.
"Ahmed ni muwezeshaji na mtoaji mafunzo mkuu wa vijana wa Kiislamu wa Kenya anayewatayarisha vijana hao kufanya vitendo vya uasi nchini Somalia," ilisema kamati hiyo katika ripoti yake iliyotolewa tarehe 23 Agosti.
"Anatoa msaada wa vitu kwa makundi yenye misimamo mikali nchini Kenya (na kwengineko Afrika ya Mashariki)," ilisema taarifa hiyo. "Kupitia safari zake za mara kwa mara katika ngome za al-Shabaab nchini Somalia, ikiwemo Kismayo, ameweza kuwa na mafungamano makubwa na wanachama wa ngazi za juu wa al-Shabaab."
"Ahmed amehubiri katika misikiti ya Mombasa kwamba vijana wa kiume lazima waende Somalia, kufanya matendo yenye mtazamo wa siasa kali, kupigana kwa ajili ya al-Qaeda na kuwaua raia wa Marekani," kwa mujibu wa ripoti hiyo.
Hadi mwaka 2010, Ahmed amefanya kazi kama mtoa mafunzo na muwezeshaji kwa ajili ya al-Shabaab katika eneo la Majengo mjini Mombasa, ilisema ripoti hiyo.

No comments:

Post a Comment

KARIBU