Meneja wa Tanesco kanda ya
Temeke,Richard Mallamia akiwaonyesha waandsishi wa habari mita
iliyochezewa na kuunganishwa umeme kinyume na mfumo wa kawaida ilikuiba
umeme kwenye duka moja eneo la Kigamboni ambapo zoezi la kukamata wezi
wa umeme linaendelea.
Mafundi wa Tanesco wakipitia pita iliyokuwa ikitumika kwa kuiba Umeme.
Mfanyabishara
duka na migahawa ya eneo la Kigamboni Jamal Hassan, akipanda kwenye
gari la Tanesco kanda ya Temeke ili kumpeleka kwenye kituo cha polisi
kutoa maelezo ya kwanini anaiba umeme.
Picha/Habari na Said Powa wa Globu ya Jamii.
SHIRIKA
la Umeme Tanesco kupitia kanda zake maalum za Ilala na Temeke jana
limeendelea na operesheni zake za kukamata wezi wa umeme wanaochezea
mita na wanaojiunganishia bila ya utaratibu maalum.
Wakizungumza
kwenye operesheni hiyo kwanyakati tofauti Mameneja hao walieleza namna
operesheni hizo zinavyosaiia kuwakamata wahalifi wa mita za umeme na
kumekuwa na ufanisi mkubwa tangu kuanza kwa zoezi hilo.
Meneja
wa kanda ya Ilala Mhandisi Athanasius Nangalia, mesema tangu zoezi
hilo limeanza mwezi mmoja uliopita wamefanikiwa kukagua wateja 4700 na
kufanikiwa kukamata wezi wa umeme 51 ambao kutokana na faini walizo
lipa wamefanikiwa kukusanya shilingi 45 Millioni.
Aidha
Nangali alifafanua kua pamoja na ukusdanyaji huo pia waligundua watu
wanaojiunganishia umeme bila ya utaratibu kwa kujiwekea nguzo zao
wenyewe lakini wamedhibiti vitendo hivyo kwa kukamata nguzo 18 kwenye
maeneo mbalimbali ya Ilala.
Aidha
kwenye zoezi lililoendelea jana eneo la Upanga liliambatana na vituko
kutoka kwa wenye nyumba baada ya kujifungia ndani na kukataa wakaguzi
hao wasiingie ndani ya nyumba hizo hata hivyo waliamua kubandika ujumbe
kwenye mageti hayo unaoeleza namba za mwisho za mita zilizo somwa na
zilizopo sasa.
KWA
UANDE WA Temeke zoezi hilo limefanyika eneo la kigamboni na
kufanikisha kutiwa mbaroni kwa watu watatu ambao wanatuhumiwa
kujihusisha na wizi wa umeme.
No comments:
Post a Comment