..

..
.

Saturday, 28 July 2012

POLISI, MSAMA WANASA WATU WANANE WANAOIBA KAZI ZA WASANII NCHINI

MKURUNGEZI wa Kampuni ya Udalali ya Msama,  Alex Msama  akionesha leo jijini Dar es Salaam, CD zenye nyimbo za wasanii walizokamatwa nazo watu 8 baada ya kudurufu kazi hizo za wasanii zenye dhamani ya milioni 25, Watuhumuwa hao wapo katika Kituo cha Polisi Buguruni, Dar es Salaam.
 Msama akionesha cd hizo
 Majina ya watu 8 waliokamatwa wakiuza CD hizo. PICHA ZOTE NA KAMANDA MWAIKENDA

MKURUNGENZI wa Kampuni ya Udalali ya Msama,  Alex Msama  akishirikiana na  Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata watu 8 baada ya kudurufu kazi za wasanii zenye thamani ya sh.milioni 25.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Msama alisema wiki iliyopita walianza zoezi la kukamata watu wanaozidurufu kazi za wasanii mbalimbali ambazo wanauza kwa faida yao.

Msama alisema wakiwa maeneo ya Buguruni sheli, walifanikiwa kuzikamata kazi hizo zikiwa zinauzwa kwa bei ya chini.Alisema kuna baadhi ya kazi hata mtaani hazijaanza kutoka lakini wao wanazo na wakiuza kwa shilingi 1000 kila moja.

"Tumekuta kazi mbalimbali kama vile za muziki wa Injili, Movies, nyimbo za bendi muziki wa ndansi na taarab" alisema Msama.Alisema licha ya kukamata CD hizo za kusikiliza na kuonesha ilifanikiwa kukamata mashine moja ya kudurufu.

Msama alisema katika zoezi hilo waliwakamata watu nane wakiwa wanauza kazi hizo.Waliokamatwa ni Halfan Bakari, Hassan Bakari,Hemed Mohamed, Patrick Peter, Hashraf Rajab, Mkoya Peter na Khamis Athuman.

No comments:

Post a Comment

KARIBU